Michezo

Manchester United yamsajili mchezaji huyu kutoka Atalanta ya Italia

Mkataba wa kiungo huyo aliye na umri wa miaka 18- unajumuisha £18.2m za ziada pamoja na mkataba utakaodumu hadi Juni 2025, na chaguo la mwaka mmoja wa ziada.

United ilifikia uamuzi wa kumsajili Diallo mwezi Oktoba.

“Baada ya kumfuatilia mimi mwenyewe, Naamini ni mmoja wa wachezaji chipukizi wa kutegemewa katika mchezo wa kandanda,” alisema meneja wa Old Trafford Ole Gunnar Solskjaer.

“Itamchukuwa muda kutulia lakini kasi yake, mtazamo na uwezo wake wa kuchenga utamweka katika nafasi nzuri ya kujiimarisha.

“Ni mchezaji alley na sifa zote zinazohitajika kuwa mchezaji muhimu wa Manchester United miaka zijazo.”

Diallo ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa chini ya masharti mapya ya baada ya -Brexit.

Nyaraka za kufanikisha uhamisho wake ziliwasilishwa muda mfupi baada ya saa sita usiku wa mwaka mpya na ziliidhinishwa siku hiyo hiyo.

Alihitaji idhini ya bodi inayosimamia soka kabla ya kuomba visa ya Uingereza, ombi ambalo aliwasilisha mapema wiki hii mjini Rome.

Diallo atasafiri hadi England punde ombi lake litakapoidhinishwa na hatahitajika kuala karantini kwani alikuwa sehemu ya ‘bubble’ ya Atlanta.

“Makocha wamekuwa wazuri kwangu tangu niliposainiwa, tumekuwa tukiwasiliana mara kwa mara na tayari wamenipa ushauri mzuri,” alisema Diallo.

“Nimekuwa na muda wa kujiandaa kwa ajili ya uhamisho huu, kimwili na kiakili na nimefanya mazoezi kwa bidii kuwa tayari kujiunga na klabu hii kubwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents