Michezo

Manchester United yapiga marufuku mashabiki kuingia na Ipad na Laptop Old Trafford

Klabu ya soka ya Manchester United imepiga marufuku mashabiki kuingia na ‘Tablets’ na komputa za ‘Laptop’ kwenye uwanja wake wa nyumbani Old Traford katika msimu huu.

Old Trafford

Taarifa kwenye mtandao wa klabu hiyo imesema, marufuku hiyo itahusisha ‘Tablet’ kubwa na ndogo pamoja na vifaa vingine vikubwa vya elektroniki, isipokuwa ‘Smartphones’ zinaruhusiwa ila kwa masharti fulani.

Klabu hiyo imesema imechukua hatua hiyo kuambatana na taarifa za kijasusi, ikiongeza kwamba kikwazo hicho kinaambatana pia na mikakakti mipya ya ukaguzi wa vifaa vya elektroini katika viwanja vya ndege.

old traff-2

Msemaji wa klabu hiyo, aliambia BBC kwamba imechukua hatua hiyo baada ya kupokea ushauri lakini hakusema ushauri huo unatoka kwa nani.

Aliongeza kwamba wasiwasi kuwa klabu hiyo haitaki mashabiki kurekodi video za mechi zinapokuwa zinaendelea na kuwazuia mashabiki wengine kutizama mechi, hauna msingi.

Msemamji wa ligi ya Uingereza naye amesema kwamba wao hawajahusika kivyovyote na marufuku hiyo.

Source: BBC Swahili

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents