Mandela afanyiwa upasuaji uliomalizika salama

610x350

Rais wa zamani wa Afrika Kusini ambaye alilazwa hospitali hivi karibuni, jana amefanyiwa upasuaji uliomalizika salama.

Mandela alikuwa akisumbuliwa na maambukizi kwenye mapafu yake.

Msemaji wake Mac Maharaj amesema Mandela alifanyiwa upasuaji wa kuondoa vitu viitwavyo ‘gallstones’.

“Upasuaji ulifanikiwa na Madiba anaendelea vizuri. Madaktari waliamua kushughulikia maambukizi kwenye mapafu kabla ya kufikiria lini wangeshughulika na gallstones,” alisema Maharaj.

Maharaj alisema vipimo vilivyofanyika baada ya Mandela kulazwa December 8 vilionesha kuwa alikuwa na ambukizi sugu kwenye mapafu na hivyo kufanya kuwepo kwa gallstones.

Aliongeza kuwa madaktari hawajasema lini ataruhusiwa kutoka hospitali.Mandela (94) alipelekwa hadi Pretoria kutoka nyumbani kwake Qunu, Eastern Cape.

Kukaa hospitali kwa Mandela awamu hii kumechukua kipindi kirefu zaid tangu mwaka 2001, alipofanyiwa matibabu ya radiotherapy baada ya kupatikana na ‘prostate cancer’ alipokuwa na miaka 83.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents