Burudani

Mandojio afungwa Singida?!

Ni masikitiko kwa wasaniii na jumuiya ya Bongo Flava kwani mchizi aliyepandisha wazimu kwa ngoma ya ‘Nikupe Nini’ a.k.a ‘Kanikamulie maji ya ndimu nina kiu koma’, Joseph Michael  ‘Mandojo’ inasemekana yupo nyuma ya nondo Singida.

Habari zisizothibitishwa zimetufikia Bongo5 kuwa msanii huyo amefungwa kwa miaka miwili jela lakini bado haijabainika kisa cha kupelekwa ubayani.

Alipoulizwa msanii mwenza wa Mandojo, Precious Juma ‘Domokaya’ last saturday aliimegea kwamba hata yeye ishu hiyo bado hajaipata fresh, anachojua ni kwamba mchizi yuko nyumbani kwao Manyoni, Singida kwa ajili ya matatizo ya kifamilia likiwemo lile la kufiwa na baba yake mzazi.

“Mi pia sijui chochote kuhusu hilo kwa sababu sijapata simu au taarifa yoyote kutoka huko, siwezi kulizungumzia hilo sana,” alisema Domo.

Tangu wiki iliyopita tumekuwa tukipokea simu na SMS za kumwaga kuhusu habari ya mchizi kwamba hana uhuru wa kawaida kama raia wa Tanzania.

Wasanii mbalimbali wakubwa pia walimwaga data kwamba Mandojo ameingia kifungoni kwa kosa la kupigana na washikaji wengine wa pande hizo.

Mandojo akiwa na Domokaya, walitikisa soko la Bongo Flava kati ya mwaka 2003 na 2004, walipotoka na ngoma ‘Nikupe’, ‘Wakafyatua Dingi’, ‘Wanoknok ft Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Taswira ft ‘Inspector Haroun’, na nyinginezo kali.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents