Michezo

Mane akiri kutopata muda wa kupumzika kwa miaka 7 sasa “Sina muda wa kupumzika, nacheza muda wote”

Nchini Uingereza mwezi Agosti ni wakati wa mapumziko na familia hutumia muda huo kujumuika pamoja baada ya shule kufungwa.

Sadio Mane

Lakini kwa wachezaji wa ligi kuu ya England mambo ni tofauti, wachezaji wamerejea kazini huku kukiwa na hofu huenda wasipate kupumzika kwa karibu miezi 12.

Mchezaji wa Liverpool Sadio Mane amegusia suala hilo akisema hajapumzika vya kutosha kwa miaka saba, baada ya kutumia mwezi wote wa Julai kuisaidia Senegal katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Wachezaji wengi wa Premier League walikuwa mapumzikoni baada ya mechi ya mwisho ya ligi hiyo Jumapili ya Mei 12.

Hata hivyo baadhi yao walichelewa kwenda likizo hasa wachezaji wa Manchester City na Watford ambao walishiriki fainali ya kombe la FA wikendi iliyofuata.

Vikosi vya Liverpool na Tottenham pia vilishiriki fainali ya Champions League iliyochezwa mjini Madrid Juni mosi.

Na hiyo ilikuwa kabla ya michuano ya Nations League, Copa America na Kombe Mataifa ya Afrika (AFCON).Sadio ManeSadio Mane

Mane, alicheza jumla ya mechi 57 nyumbani, Ulaya na zingine za kimataifa katika kipindi cha zaidi ya miezi 11 katika msimu wa mwaka 2018-19.

Hii inamaanisha nyota huyo wa kimataifa wa Senegal wa miaka 27 alianza mazoezi ya msimu mpya Jumatatu ya Agosti 5- siku 17 baada ya kufanya mazoezi yaliyopita

“Nadhani niko tayari,” alisema Mane aliyejipata katika hali kama hiyo miezi 12 iliyopita baada ya kucheza Kombe la Dunia nchini Urusi.

“Sina muda wa kupumzika. Nimekuwa nikicheza kwa muda mrefu. Sijawahi kwenda likizo kwa zaidi ya siku 20 katika kipindi cha miaka saba lakini nimezoea. Sasa niko tayari. Nipo hapa sasa twende kazi.”

Wachezaji wenzake Mane kama vile Alisson, Mohamed Salah, Roberto Firmino na Naby Keita ni baadhi ya wachezaji wa ligi ya Premia walioshiriki mashindano ya msimu wa joto hatua iliyowafanya kukatiza likizo zao kabla ya ligi mpya msimu mpya kuanza.

Lakini kwa wachezaji ambao hawakushiriki mashindano walitarajiwa kufanya mazoezi baada ya msimu kwisha ili kujiimarisha huku wengine wao wakilazimika kwenda na wakufunzi wa kibinafsi likizo.

Kandarasi ya wachezaji inasema nini kuhusu likizo?

Kwa mujibu wakandarasi ya Ligi ya Premia/Soka ya Ligi ya Uingereza, wachezaji wanastahili kwenda likizo ya “wiki tano ya kulipwa wakati ambao utaamuliwa na klabu- ikiwa mchezaji yuko katika kikosi cha kwanza au anahitajika kushiriki mechi ya kimataifa”.

Mazingira ya kazi yao haiwaruhusu kusugeza mbele likizo “Klabu hata hivyo haitamzua mchezaji kuchukua angalau likizo ya wiki tatu bila msingi”.

Hilo lingefakiwa ingelikuwa jambo la kuvutia sana kwa Mane, na mshambuliaji wa Tottenham Son Heung-min ambaye alicheza mechi 78 na kusafiri zaidi ya km110,000 kuiwakilisha Korea Kusini mwaka uliopita.Son Heung-min

Mshambuliaji wa Tottenham, Son Heung-min

Muungano wa kimataifa ya data ya wachezaji ilionesha kuwa wachezaji mashuhuri 16 walicheza karibu mechi 80 katika msimu wa mwaka 2018-19.

Wachezaji wanapigika sana?

Likizo ya msimu wa joto huchukuliwa kama likizo ya siku kuu ya Krismasi na wachezaji Barani Ulaya, na baadhi yao hujivinjari mbali na familia na marafiki zao katika migahawa mikubwa kabla ya michezo ua siku ya kufungua zawadi.

Jedwali lisilokuwa na muda wa mapumziko limekosolewa sana kocha wa Liverpool Jurgen Klopp na mwenzake wa Manchester City, Pep Guardiola.

Klopp alisema: “Ikiwa hatutajifunza jinsi ya kuwasiliana na wachezaji kwa njia bora, wakati wa mashindano, basi huenda tukaangamiza huu mchezo mzuri. Kwa sababu bila wachezaji, hakuna litakalofanyika.”

Guardiola anasema michezo ya wakati wa sherehe “inawamaliza” wachezaji wake japo msimu huu angalau watapumzika wikendi moja mwezi Februari, hatua ambayo Shirikisho la Soka limesema ni “muhimu”.

Lakini kabla ya kuangazia zaidi maslahi ya wachezaji, ni vyema kutilia maanani kuna baadhi ya kazi ambazo watu wanachukua muda mrefu zaidi ofisini ikilinganishwa na mazoezi ya kandanda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents