Michezo

Maneno aliyosema Drogba baada ya timu yake kupata ushindi dhidi ya Toronto FC

Mchezaji wa Klabu ya Montreal Impact Didier Drogba usiku wa kuamkia leo timu yake imeibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Toronto FC kwenye fainali ya ukanda wa mashariki.

drogba

Baada ya mchezo huo wa kwanza wa fainali ya ukanda wa mashariki kumalizika, Drogba aliwaambia waandishi kuwa huo ndio ulikuwa ni mchezo wake wa mwisho kwenye uwanja wa nyumbani wa Montreal.

“Bado kuna mechi 1 au 2 zilizobaki. Mechi ya wiki ijayo ni muhimu sana.

Kila mmoja anafahamu kuwa hii ilikuwa mechi yangu ya mwisho hapa (Uwanja wa nyumbani). Sasa acha tuelekeze akili zetu katika nusu fainali.” amesema Drogba.

Mshindi wa nusu fainali hiyo atacheza mechi ya fainali ambayo itapigwa Disemba 10.

Drogba ambaye amejiunga na klabu hiyo Montreal Impact mwaka 2015 akitokea Chelsea, na kufanikiwa kucheza mechi 33 akifunga goli 27 kunako timu hiyo inayoshiriki MLS.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents