Habari

Maneno ya Mh. Freeman Mbowe kwa Watanzania baada ya kufiwa na kaka yake

Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amewashukuru wote walioenda kuwaona baada ya kusikia kifo cha kaka yake, Marehemu Henry Mbowe na kufika kanisani kwaajili ya kuuaga mwili wa kaka yake huyo.

Mbowe ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii, amesema hata wale waliompigia na kutoa pole amepokea pole zao kwa mikono miwili.

Kwa mara nyingine nawashukuru wote mliotukimbilia kama familia baada ya kusikia kifo cha kaka yangu mpendwa sana Henry, mlioweza kufika nyumbani au pale Kanisani Usharika wa Kunduchi Dar es salaam, kwa ajili ya kumuaga kaka na kutoa heshima za mwisho kwa wale ambao wasingepata nafasi ya kusafiri nasi kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko hapo kesho nawashukuru sana.

Wengine wamenipa pole kwa kwa kunipgia simu kwa sababu wasingeweza kufika kwa wakati kutokana na shughuli mbalimbali za kila siku zinazotukabili sisi kama wanaadamu, nimepokea pole zenu kwa mikono miwili ahsanteni sana.

Nawashukuru sana sana wote, tunategemea Mungu akipenda kesho tutampumzisha kaka katika nyumba yake ya milele nyumbani Machame kijijini Nshara. Nawashukuruni Mungu awabariki sana ndugu zangu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents