Michezo

Maneno ya mtoto huyu yamtoa machozi Ronaldo hadharani, akiri kuimisi zaidi Real kuliko Man United, aahidi kurudi Madrid (+video)

Usiku wa jana siku ya Jumatatu mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo alitwaa tuzo ya Marca’s Legend award nchini Hispania.

https://www.youtube.com/watch?v=Ge3Vvf_L6O0

Ronaldo alijikuta akitokwa na machozi mara baada ya mtoto mmoja kumweleza kuwa alijisikia vibaya sana alipomuona akiondoka Real Madrid na nyota huyo kujibu hata yeye pia ilikuwa hivyo hivyo na kutokwa na machozi.

Mtoto huyo alichomwambia Cristiano Ronaldo “Nilijisikia vibaya sana nilipokuona unaondoka Real Madrid,” na staa huyo kujibu “Mimi pia.”

Mbali na kukutana na rais wa klabu yake ya zamani Real Madrid, Florentino Perez lakini pia alipata nafasi ya kuzungumza mache na baadhi ya watu wakiwemo watoto ambao walikuwa wameandaliwa na Marca.

Kabla ya hapo mchezaji huyo wa zamani wa Madrid, alionyesha hisia zake namna anavyoipenda timu hiyo zaidi ya Manchester United.

“Naimisi Manchester na Madrid, lakini watoto wangu wamekulia hapa kwahiyo naimisi zaidi Madrid, hii tuzo ninakwenda kuiweka sehemu yangu ya makumbusho, Madrid ni sehemu muhimu nimetembea sana lakini kuna miji michache sana ambayo ni kama Madrid na hata sehemu kubwa ya tuzo hii nimeipata kutokana kile nilichokifanya Real Madrid.” – Amesema Ronaldo.

Cristiano Ronaldo ameongeza “Hii ni tuzo ya Kihispania na kwaheshima kubwa nakubali kuipokea. Ahsante kwa kila mmoja aliyenisaidia kupata tuzo hii na natumaini nitarejea katika jiji la Madrid hivi punde.”

“Kurudi kwangu Madrid ni kitu muhimu kwangu, kama nilivyosema na nitaendelea kusema hili ni moja kati ya majiji mazuri hapa duniani, jiji lililojaa upendo lakini pia kutokana na historia niliyoiwacha hapa. Natumaini kurejea jiiji hili la Madrid hara iwezekanavyo.”

Ronaldo anaungana na mastaa wengine kama Michael Jordan, Pele, Rafa Nadal, Novak Djokovic, Muhammad Ali, Usian Bolt, Michael Phelps, Michael Schumacher and Diego Maradona katika kuchukua tuzo hiyo. Hasimu wa Ronaldo ambaye ni mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi amewahi kuchukua tuzo hiyo mwaka 2009.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents