Habari

Maneno ya Mzee Makamba kwa Rais Magufuli ‘2020 mshindi ni CCM, wewe lala’

Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba amemuambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mwaka 2020 mshindi wa CCM hivyo amemuasa alale.

Akiongea leo katika Mkutano Mkuu wa 9 wa CCM alipopewa nafasi ya kuzungumza amesema kuwa Rais Magufuli ahitaji kwenda kwa Prof. Maji Marefu kupiga ramli kujua mshindi nani.

“Nyumba inajengwa na msingi na msingi wa CCM na nchi hii umejengwa na wazee wetu Nyerere na Karume hivyo walichokifanya wazee Mwinyi, Mkapa na wengineo ni kujenga matofali kama ambavyo amefanya Jakaya Kikwete na unavyofanya Rais Magufuli,” amesema Yusuph Makamba.

“Kwa ubatizo huu wa moto, 2020 mshindi ni CCM, wewe lala, hauhitaji kwenda kwa prof. Maji Marefu kupiga ramli kujua mshindi nani.Kuna mtu alikufananisha na nabii Nehemia lakini mimi nakufananisha na Yohana mbatizaji.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents