Maneno ya Ronaldo baada ya Ubingwa wa Uefa 2017 (Picha)
Mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo wikiendi hii alikuwa na kibarua kizito katika mji wa Cardiff pale ambapo timu yake ilipo ikabili kibibi cha torino Juventus ya Italia.
Wachezaji wa klabu ya Real Madrid wakishangilia ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya
Mara baada ya kukisaidia kikosi cha kocha Zinedine Zidane’ kutwaa kombe la klabu bingwa barani Ulaya huku akitupia magoli mawili kati ya manne waliofunga katika mchezo huo.
Ronaldo alisema, “Namba iliyonyuma ya mgongo wangu haidanganyi”
“Hii ni moja ya kumbukumbu zangu bora katika tasnia yangu imezoeleka nikisikika nikisema hivi kila mwaka ,” alisema.
“Watu wamezoea kuni kukosoa kila siku ila najua kwa sababu namba haidanganyi.”
“Hii klabu ipo ndani ya moyo wangu na tunakwenda kuufurahia ushindi huu. Leo nisiku yaa historia ya kweli kwa Real Madrid na mashabiki wote wa Madrid.”
Nae kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos ambae kwa sasa ameshinda Champions League mara ya tatu akiwa na klabu ya Real pamoja na Bayern Munich, alisema hapo ndipo thamani ya Ronaldo kwa Zidane’s inapo onekana .
“Siku tarajia, hili ni kama swala ambalo aliwezekani kutetea ubingwa huu, ni vigumu sana kushinda taji hili kwa mara nyingine nfululizo,”.
“Kila mtu anafahamu kuwa Cristiano ni muhimu. Kama timu tulicheza vizuri katika hatua ya robo fainali, nusu fainali na fainali lakini uanapo mtu wa kuhakikisha mnafunga magoli na yeye aliweza kufanya hivyo. alisema Toni Kroos.
Mchezaji Cristiano Ronaldo akitangazwa kuwa man of the match , na Kocha wake wazamani ” Sir Alex Ferguson , huku mchezaji huyo akiwa na mtoto wake
Magoli aliyofunga katika kila kipindi cha mchezo yanamfanya mreno huyo kufikisha jumla ya magoli 105 hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo klabu ya AC Milan mwaka 1990 baada ya kushinda na kutetea tena ubingwa.
Juventus ambayo ilionekana kufanya vizuri katika dakika 45 za kipindi cha kwanza, Ronaldo alifungua lango la timu pinzani kwa kushinda goli la kwanza kwa upande wa Madrid kabla ya mchezaji wa Juve, Mario Mandzukic’s kuisawazishia timu yake.
Mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya klabu ya Real Madrid wakishangilia ubingwa wao baada ya kumngu Juventus kwa jumla ya magoli 4 kwa 1
Lakini Real walikuja kwa kasi kupitia wachezaji wake Casemiro, Ronaldo pamoja na Marco Asensio nakuifanya klabu hiyo kujinyakulia taji lake la 12 michuano ya Ulaya na latatu katika misimu minne
Ronaldo ndie mchezaji ambae amefunga angalau mara mbili katika mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya hatua ya robo fainali magoli (20), nusu fainali (13) na fainali (4) kuliko yeyote .
Mchezaji huyu ameshinda mataji manne ya klabu bingwa barani ulaya na kwa sasa ameshinda zaidi ya magoli 11 katika mashindano haya na kumshinda mpinzani wake wa karibu Barcelona Lionel Messi.
Picha zifuatazo ni Mapokezi ya klabu ya Real Madrid mbele ya mashabiki wao nchini Hispania
BY HAMZA FUMO