Habari

Maneno ya Spika Ndugai baada ya mahakama kutupilia mbali ombi la Lisu kuhusu kupokonywa Ubunge – Video

Maneno ya Spika Ndugai baada ya mahakama kutupilia mbali ombi la Lisu kuhusu kupokonywa Ubunge - Video

Baada ya Mahakama kutupilia mbali madai ya kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Jumanne.
Baada ya Mahakama kutupilia mbali madai ya kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Ndugu Tundu Lissu, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameyasema haya Bungeni.

Ikumbukwe kuwa hivi leo mapema.

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam,  imetoa maamuzi kesi ya maombi ya kupinga kuvuliwa ubunge iliyokuwa imefunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, kwa kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo

Maamuzi ya kesi hiyo yametolewa leo Septemba 9, 2019 na Jaji Sirillius Matupa na kudai kwamba kesi hiyo ni ya kikatiba hivyo inapaswa kufunguliwa kwa mfumo wa kesi ya uchaguzi na si kwa mfumo ambao alikuwa ameutumia,  huku pia akieleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kutengua ubunge wa Mbunge Julius Mtaturu aliyeteuliwa hivi karibuni.

Kesi hiyo namba 18 ya mwaka 2019, Lissu aliiomba Mahakama kibali cha kufungua shauri la kupinga taarifa ya Spika wa Bunge Job Ndugai ya kukoma ubunge wake,  ambapo Mahakama imetupilia shauri hilo.

Kwa upande wa waleta maombi katika kesi hiyo, wameahidi  kwamba watajipanga upya ili  kufungua kesi ya uchaguzi na hatimaye  kuipata haki yao. Hadi sasa Mbunge mteule wa CCM Julius Mtaturu, ataendelea kuwa Mbunge wa Singida Mashariki.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents