Burudani

Maneno ya Wastara kwa Sajuki ‘nitakuwa na wewe kokote niendapo’

Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Wastara ameupokea mwaka mpya wa 2018 kwa kumkumbuka aliyekuwa mumewe Marehemu Juma Kilowoko Sajuki .

Marehemu Sajuki na Wastara

Wastara amesema kila mwaka tarehe kama ya leo (Januari 1) huwa anaitumia kuangalia picha za Sajuki ili kujipa faraja na kitendo hicho kwa sasa kimekuwa kama desturi huku akiahidi kuwa kamwe hatoacha kufanya hivyo.

Kama kuposti picha zako kila mwanzo wa mwaka huwa kunaniletea shida na matatizo katika maisha yangu Basi wacha tu yanikute niko tayari kuyapokea lakin hakuna wa kusitisha zoezi hili katika maisha yote mpaka nakufa,“ameandika Wastara kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wastara amedai kuwa anajua kitendo cha kufanya hivyo kinawaumiza baadhi ya watu lakini yeye anaamini kuwa ni faraja kwake na anafanya hivyo ili kuwa pamoja na marehemu kiroho.

“Nitakuwa na wewe kokote niendapo japo kiroho inanitosha na kujiona tupo pamoja kwa siku chache ukinipa ile furaha uliyoondokana nayo Mungu akupe kauli thabiti akuondosheee adhabu na mchanga mzito kaburini kwako”ameandika Wastara.

Marehemu Juma Kilowoko Sajuki alifariki Januari 2, 2013 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents