Manji Amdisi Mengi Live

Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Group bwana Yusuf Manji, hivi karibuni amesema kuwa kamwe hatasita kusema ukweli pale anapoona vyombo vya habari vinakiuka maadili ya kazi zake na kumtaka Mkurugenzi wa IPP, Reginald Mengi asijifananishe na Mungu mtu

Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Group bwana Yusuf Manji, hivi karibuni amesema kuwa kamwe hatasita kusema ukweli pale anapoona vyombo vya habari vinakiuka maadili ya kazi zake na kumtaka Mkurugenzi wa IPP, Reginald Mengi asijifananishe na Mungu mtu kwa kuogopwa na kila mtu.



Aliyasema hayo alipokuwa akizungumzia mamuzi ya kamati ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ilitoa ushindi kwa Independent Television (ITV) dhidi ya Yusuf Manji aliyekuwa akilalamika kwamba kituo hicho cha luninga hakikumtendea haki katika taarifa yake ya habai iliyorushwa Agosti 22, 2007.



Bwana Mengi alizungumza mengi na waandishi wa habari akimshutumu Manji kwa kutofika wakati hukumu inatolewa na kwamba amempotezea muda kutokana na kiburi chake na kumtaka asome sheria kabla ya kupeleka malalamiko kwenye ngazi za juu.



“Namshangaa Bwana Mengi kwa kupenda kuonekana kwenye televisheni na kuanza kuongelea mambo yasiyomhusu, mimi niliishitaki taasisi ya ITV na si Mengi hivyo nilitegemea kuona mtendaji mkuu wa ITV analiongelea hilo na si yeye,” alisema Manji.



Manji amesema kuwa vyombo vya habari vya IPP ni kama vilivyo vyombo vingine hivyo hataogopa kusema ukweli pale atakapoona chombo cha habari kinapindisha maadili ya kazi yake.



Aliongeza kwa kusema kuwa, Mengi hayupo juu ya sheria yupo kama watu wa kawaida na si vizuri mtu kujiona kama yeye ndiye mwenye haki kwani kila mtu ana haki ya kushitaki kwa kitu chochote pale atakapoona ametendewa kinyume na sheria kwani kila mtu anastahili kupata iliyo haki yake.


 


Amesema katika hukumu iliyotolewa na Kamati ya Mahudhui na Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilimpongeza kwa kuishitaki ITV na kuwataka watu wengine waige mfano huo pale wanapoona hawajatendewa haki na vyombo vya habari. Pia ilitoa onyo kali kwa ITV kutunza vizuri mikanda ya kurekodia kwa ajili ya kutumia kwenye ushahidi wowote.


 


Katika hukumu hiyo pia TCRA ilisema kauli iliyotolewa na Sheikh Khalifa katika mkutano na waandishi wa habari ikidai kwamba kampuni ya Quality Group ilipata kiwanja cha BAKWATA isivyo halali, ilichapishwa na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo ITV na kwamba upande wa madai ulikuwa na haki ya kujibu tuhuma hizo.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents