Habari

Manji aomba msamaha baada ya kuchelewa mahakamani

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Cyprian Mkeha amemuuliza mfanyabiashara Yusufu Manji kwa nini amechelewa mahakamani wakati walipaswa kuanza saa tatu asubuhi.

Manji

Kutokana na swali hilo, Manji aliomba msamaha kwa kuchelewa na kwamba alipitia hospitali kabla na aliwasiliana na wakili wake alimueleza kuwa hakimu yupo kwenye kikao.

Swali hilo lilikuja baada ya kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili Manji kushindwa kuendelea na kupelekwa hadi Septemba 25, 2017.

Ni baada ya Wakili wa Manji, Hajra Mungula leo Jumatatu kueleza kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi na kwamba wapo tayari.

Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis alieleza kuwa yeye anataka kusafiri mchana na kwa kuwa kesi imechelewa kuanza kusikilizwa hawezi kuendelea.

Hakimu Mkeha naye alisema anaenda katika kikao mchana huo, hivyo Wakili Mungula aliomba kesi hiyo ipangiwe siku tatu mfululizo, kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi Septemba 25, 26 na 27, 2017.

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo awali walidai watawaita mashahidi wasiozidi 10 kutoa ushahidi katika kesi hiyo lakini wakatoa watatu na kufunga ushahidi wao.

Manji yeye anatarajia kuwaita mashahidi 15 na ametoa mmoja ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Manji alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 ambapo anadaiwa kuwa , kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.0

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents