Habari

Manji asakwa na uhamiaji kwa kuajiri wafanyakazi 25 toka nje ya nchi wasiokuwa na vibali

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga na mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Group akiwa bado amelazwa katika taasisi ya Moyo ya JKCI, Kikosi cha uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza kumchukulia hatua kwa kosa la kuajiri wafanyakazi toka nje ya nchi wasiokuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.

Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Dar es salaam, John Msumule

Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne hii, Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Dar es salaam, John Msumule amesema wakimkamata watampandisha mahakamani ili kujibu shtaka linalomkabili.

“Tumekagua passport 126, lakini 25 zinamakosa, tumechambua passport 25 hawana vibali vya kufanya kazi nchini,” alisema afisa huyo. “Kwa hiyo wanafanya kazi kinyume na utaratibu, wote hawa hatua zitachukuliwa kwa kupelekwa mahakamani,”

Aliongeza, “Lakini labda niseme ukweli hawa hawatapelekwa peke yao mahakamani lazima na Yusuph Manji ambaye ndiye mwajiri wa hawa watu, ambaye ndiye mmiliki wa kampuni, lazima afikishwe mahakamani kujibu shtaka la kuajiri watu wasio na vibali. Jana tulikuwa tumkamate alale mahabasu ili afikishwe mahakamani. Bahati mbaya wakati tunafanya zoezi la kwenda kumkamata, tukapewa taarifa kwamba amelazwa hospitalini mpaka sasa, mara tu atokapo aripoti ofisi hii tumuunganishe kwenye kesi hii ya kuajiri watu wasio na vibali,”

Alisema hawatojali pesa zake wala utajiri kwani atawekwa ndani kwajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents