Mitindo

Manju Msita aalikwa Mozambique

Manju Msita Aalikwa Mozambique Fashion Week

Mbunifu wa mavazi na mitindo maarufu hapa nchini, Manju Msita, anatarajiwa kuwakilisha Tanzania katika onyesho la wabunifu wa mavazi na Mitindo jijini Maputo Msumbiji. Onyesho hilo ambalo linakwenda kwa jina la Mozambique Fashion Week linatarajiwa kufanyika mjini Maputo kuanzia tarehe 6 mpaka 11 Desemba, 2010.

Mwaliko huo wa mbunifu huyo ni kutokana na matunda ya ushirikiano wa kikazi baina ya Swahili Fashion Week na Mozambique Fashion Week ambao ulianza mwaka 2009 ambapo wabunifu Adeila na Sheila Tique kutoka Msumbiji walikuja Tanzania na Janila Vera Swai alikwenda msumbiji kuonyesha mavazi yao.

Manju Msita Aalikwa Mozambique Fashion Week

Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari waandaji wa Mozambique Fashion Week wamesema kwamba mwaka huu mbunifu Marinella Rodriguez aliiwakilisha Msumbiji katika Swahili Fashion Week hivyo ni furaha kwao kumualika Manju Msita katika Mozambique Fashion Week.

Manju akiongelea mwaliko huo alisema, ‘Ni furaha kubwa kwangu kupata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika wiki hiyo ya ubunifu Mozambique kwani ni moja ya tukio kubwa la ki ubunifu na mitindo barani Afrika’ .

Aidha Manju alichaguliwa na Producer wa kimataifa wa maonyesho ya ubunifu Jan Malan Umzingeli akishirikiana na waandaji wa Swahili Fashion Week kuchagua nani wa kuiwakilisha Tanzania katika wiki hiyo ya ubunifu.

Akizungumzia hatua hiyo mbunifu wa mavazi ambaye pia muandaaji wa Swahili Fashion Week Mustafa Hassanali amesema hiyo ni hatua kubwa ya ushirikiano na sio tu ya kisiasa bali ya kiutamaduni na kiubunifu.

‘Nafikiri hatua ya kumwalika Manju ni ishara ya ushirikiano thabiti baina ya kati ya nchi zetu mbili,’ alimalizia Hassanali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents