Michezo

Manuel Neuer atolewa katika kikosi cha Ujerumani

Kipa wa klabu ya Bayern Munich Manuel Neuer ametolewa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ujerumani kufuatia kusumbuliwa na maumivu ya shavu la mguu (Calf). Nafasi yake imechukuliwa na kipa wa klabu ya PSG, Kevin Trapp.

Ujerumani ambao ndio Mabingwa wa Dunia jumatano hii watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya England huko Dortmund, na jumapili watacheza na Azerbaijan ikiwa ni mechi ya kufuzu kombe la Dunia 2018,Russia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents