Michezo

Maofisa wa FIFA kutua nchini sakata la TFF

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) muda wowote kuanzia sasa litatuma maofisa wake kuja nchini kufuatilia tuhuma za utakatishaji fedha alizonazo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.

Rais wa TFF,Jamal malinzi(katikati), makamu wa klabu ya Simba,Geofrey Nyange ‘Kaburu’(kulia) na katibu Mkuu wa TFF,Mwesigwa Celestine (kushoto)

 

Malinzi na wenzake ambao ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mkurugenzi wa Fedha wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Baada ya kusomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbord Mashauri katika kesi yao namba 213, watuhumiwa hao walinyimwa dhamana na kupelekwa mahabusu hadi kesi yao itakaposikilizwa tena keshokutwa Jumatatu.

Rais wa TFF, Jamal malinzi (katikati)

Akizungumza na Championi Jumamosi, Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia alisema Fifa tayari ina taarifa za viongozi hao wa TFF kukamatwa na kupandishwa kizimbani kisha kwenda mahabusu.

“Fifa itatuma maofisa wake muda wowote kuanzia sasa na wakifika nchini tutakutana nao katika kikao Jumanne ijayo ili waweze kujua undani wa tuhuma zote walizonazo wenzetu, nadhani kila kitu kitakuwa sawa baada ya hapo.

“Sisi kama TFF hatuwezi kuzungumza lolote kuhusu kukamatwa kwa watu hawa kwani tayari shauri lipo mahakamani,” alisema Karia ambaye pia anagombea nafasi ya urais wa TFF katika uchaguzi utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.

Ni wazi kwamba kuna ugumu wa Malinzi kuwahi usaili kwani leo ndiyo mwisho na yeye atafikishwa mahakamani keshokutwa Jumatatu.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents