Burudani

Maoni: Hawa ni rappers 5 bora Tanzania katika muongo mmoja uliopita

Kumekuwa na mijadala na mabishano juu ya nani anastahili kuwemo kwenye kundi la top rappers katika industry ya Bongo Rap kwa miaka kumi iliyopita. Ifuatayo ni orodha ya top 5 rappers kwa mujibu wa utafiti usio rasmi

Vigezo vilivyotumika ni kama consistency ya msanii,idadi ya hits songs,shows,fan base n.k.

1. Profesa Jay

Ukiwauliza mashabiki kumi wa muziki wa bongo fleva achilia mbali rap, kama sio kumi wote basi watu nane watamtaja Profesa kama mmoja wa wasanii bora wa rap kuwahi kutokea. Katika miaka kumi iliyopita Profesa Jay si tu ametoa hits song za kutosha bali ameendelea kulinda heshima yake ya kuwa mmoja kati ya wasanii ambao ni mfano wa kuigwa miongoni mwa wasanii na ni msanii mwenye mashabiki ambao ni wasanii kupita msanii yoyote yule iwe rap au aina nyingine ya muziki katika bongo fleva. Na pengine ndio sababu hakuna aliyeshangaa kuona watu wa Mikumi wamemchagua kuwa mwakilishi wao bungeni!

2. Fid Q

Kwa mujibu wa baadhi ya mashabiki niliofanikiwa kupata maoni yao, wengi wao wanamtaja Fareed kama ni msanii anayeishi katika dunia yake mwenyewe linapokuja suala la uandishi. Pengine Fareed ni mmoja ya wasanii wachache kwenye main stream wanaokubalika na wasanii wahafidhina wa hip hop ambao wengi wao hawapo main stream. Siku za karibuni producer mkubwa na mwenye heshima kubwa kwenye muziki wa Bongo, P-Funk alimtaja kama ndIo msanii mkali zaidi wa rap duniani!
Hakuna namna unaeza acha kumtaja Fid Q unapotaja top rappers kwa miaka kumi iliyopita.


3. Mwana FA

Pengine ukimtoa Profesa katika list hii, Mwanafalsafa ndIo msanii aliyeanza kuhit kwenye mainstream kuliko wengine. Tangia hapo hajawahi kuondoka masikioni kwa mashabiki na kila akigusa imooo. Mwanafalsafa anatajwa kama fundi wa maneno na ni rapper ambaye anasifika kama ndio fundi wa romantic rap songs.
Katika kujaribu kupata maoni ya watu, watoto wa kike wengi walimtaja Mwana FA kama ndo msanii wa rap wanayemsikiliza zaidi labda ni kwa sababu alisema yeye na mabinti damu damu.

4. AY

Miaka mingi iliyopita nilimuona akihojiwa na kituo fulani cha TV. Katika maongezi yake alisema ana mpango wa kupeleka muziki wake kimataifa na kwa kipindi kile ilionekana ni ndoto za mchana Lakini leo tunapozungumzia Tanzania kuwa kwenye ramani ya muziki Afrika na duniani pengine hatuwezi acha kumtaja Ambwene kama mmoja ya watu wenye uthubutu na mchango mkubwa kufika hapo tulipo. Amefanya collabo kubwa za kimataifa lama P-Square,Sean Kingston,Miss Trinity na wengineo.
Pamoja na kuWa watu wengi walisema hawana uhakika kama ni rapper kutokana na kubadilika kwake,Ay alitajwa katika kila list ya kila niliyefanikwa kumuuliza.

5.Joh Makini

Nakumbuka show fulani ya Fiesta 2006 or 2007 kama sikosei,kipindi hicho akitamba na Chochote Popote Joh alifanikiwa kuteka mioyo ya watu pasipo kutarajia. Tangia hapo mwamba ameendelea kumaintain kwenye game. Uwezo wake wa kubadilika unamfanya aendeelee kujizolea mashabiki kila uchwao. Yeye na Mwana FA ndio wasanii waliotajwa zaidi na mashabiki wa kike kama ndo wasanii wanaowasikiliza zaidi kwa upande wa rap. Kwa mujibu wa AY, Joh ndo msanii pekee wa rap kuingia kwene A-list ya rappers Bongo.

List hii imeandaliwa kwa maoni yangu mimi pamoja na baadhi ya watu niliofanikiwa kuwauliza informally. Albeit Mangwair alitajwa kama msanii ambaye kama angelikuwa hai basi ni wazi angekuwepo kwenye list. Bila kumsahau Chidi Benz ambao wengi wanaamini yaliyotokea hapa katikati yamemfanya kushindwa kumaintain.

Imeandikwa na Eliezer Gibson ‘greencitynative

Instagram:@gibson_elly

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents