Burudani

Maoni: Kwa mujibu wa vigezo vya EATV Awards, Alikiba anastahili tuzo 3 alizopata

Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa muziki wa Tanzania na kwa jicho ziada, nimezifuatilia kwa kina tuzo za EATV zilizofikia kilele jana. Nimeona, kuna kuna watu wanalalamika pasipo kujua utaratibu wa tuzo hizi ukoje. Ili kuwa nominated kwenye EATV Awards, ilikuwa ni lazima kwanza msanii achukue fomu ya ushiriki ndipo aweze kuingizwa katika orodha ya wasanii watakaoshiriki.

img_9315

Jopo la EATV likafanya mchujo kupata orodha ya watu 5 ambao watapigiwa kura.

Sifahamu vigezo vyao katika kuchagua nyimbo zilizostahili kuingia katika 5 bora kwa kila kipengele, lakini ninachojua ni kuwa nyimbo zote au wasanii waliopita kwenye 5 bora wamestahili kabisa. Ukipitia habari hii, Hawa ni washindi wa tuzo za EATV 2016, Alikiba akomba tuzo 3, utagundua kuwa kuna baadhi ya watu wanalalamika kuhusu Video bora ya mwaka.

Naweza kusema labda ni kwa sababu ya hizi Team fulani na Team fulani.

Ebu tafakari kidogo kwanza. Nini maana ya kupiga kura? Ukitazama orodha ya video 5 zilizoingia, nadhani hakuna ubishi kuwa AJE ya Alikiba imefanya vizuri kushinda video zote zilizoshindanishwa naye katika kipengele cha video bora.

Achilia mbali kura alizopata Alikiba na kumfanya kuwa mshindi wa video bora, bali msanii huyu ana hazina kubwa sana ya mashabiki na wanakesha wakimpigia kura.

Tazama kidogo washiriki wa kipengele hiki:

1. Alikiba – Aje
2. Shetta – Namjua
3. Navio – Njogereza
4. Joh Makini – Dont Bother
5. Lady Jaydee – Ndi ndi ndi

Hata kwa upeo mdogo tu, kinyang’anyiro cha kipengele hiki kilikuwa ni cha watu watatu Alikiba, Joh Makini, na Lady Jaydee, ” maana kwa haraka haraka tu ndio wenye nguvu zaidi kwa Tanzania.

Hivyo kwa mtazamo wangu, Alikiba amestahili kabisa kuchukua tuzo tatu alizo pata hapo jana. Hongera sana kwa EATV kwa kuweka alama katika tasnia ya burudani Tanzania. Bila shaka tutarajie mengi zaidi mwakani maana ninaamini huu ni mwanzo tu na ni mwanzo mzuri kabisa.

Napenda niaache kwa maneno haya tu, “Tuache maneno, tuwasapoti wasanii wetu wanaofanya muziki mzuri.”

Imeandikwa na Ally Msangi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents