Burudani

Maoni: Sitaki kuamini kama TID ni ‘Rotten Apple’

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 enzi hizo nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi,masikio yangu yalisikia sauti ambayo ni ya kipekee, yenye hisia kali na yenye mvuto wa aina yake pengine kuwahi kutokea kwenye muziki wa Bongo. Nilisikia sauti hiyo kwa mara ya kwanza kwenye wimbo, Tutakukumbuka wa King Crazy GK.

Masikio yangu yaliendelea kuisikia sauti hiyo kwenye nyimbo kama Zeze, Mrembo, Siamini pamoja na Siku Kama Hizi, moja kati ya nyimbo tamu na yenye hisia kuwahi kusikika kwenye masikio yangu. Ni sauti ya Khalid Mohamed aka TID.

Nani anabisha TID sio tu kuwa ni msanii mkali, ila sauti yake huwezi kusikia angalau ikifanana hata kwa mbali na msanii yoyote kwa sasa? Unaweza ukasema TID ni full package anaweza akacheza kwa umahiri ule ule unaofanana na kuimba kwake. Kifupi TID ni moja kati ya wasanii waliokamilika kuanzia muonekano, uwezo wake wa kuimba,kupiga show,jinsi anavyoweza kuongea kwa manjonjo akichagizwa na uwezo wake mkubwa wa kuchanganya kiingereza na Kiswahili.

TID akiwa miongoni mwa wasanii wachache kipindi kile kuwa na uthubutu wa kufanya video za kiwango kikubwa walau, msanii aliyekuwa akifanya show mara kwa mara nje ya mipaka ya Tanzania ungetegemea kipindi hiki ambacho muziki wetu unatambuliwa nje ya mipaka basi awe mmoja wa wakilishi wakuu wa Tanzania. Nina uhakika pengine hizi team zisingekuwa na nguvu zilizonazo sasa, But TID is not there; anatoa ngoma hazifanyi poa, uwezo wake ni mkubwa sana bado na mfano ni chorus aliyofanya kwenye Ligi Ndogo ya Bill Nas, bado siamini kama ni ‘rotten apple.’

TID kuna mtu mmoja tu anayezuia wewe kufanikiwa, kuna mtu mmoja tu anayesababisha hatukuoni ukitajwa kuwania tunzo kubwa Afrika ukitoana jasho na kina P-Square, kuna mtu mmoja tu anasababisha sauti yako ya dhahabu ipotee kwenye masikio ya watu; mtu mwenyewe utamuona siku ukisimama kwenye kioo chako chumbani.

Bro ukishamuona huyo muulize maswali magumu, hakikisha anakujibu na wala usimuonee haya akikupa majibu huyo. Nina uhakika nothing can stop you not only to be the Top in Dar, but also in Africa, talk to him bro!

Imeandikwa na Eliezer Gibson Aka Green City Native

Facebook:Eliezer Gibson

Instargram:@gibson_elly

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents