Habari

Mapacha waliopewa asilimia 20 ya kuishi wakati wa upasuaji wao wakaribia kuanza shule

Mapacha wa Uingereza waliozaliwa wakiwa wameungana kwenye sehemu ya tumbo waliyokuwa wanatumia kabla ya kufanyiwa upasuaji wa dharura wa kuwatenganisha mnamo mwaka 2012, wanatarajiwa kuanza shule mwezi Septemba mwaka huu.

_90964463_twins4pa

Kabla ya upasuaji huo wa mapacha hao ambao wanajulikana kwa jina la Rosie na Ruby walikuwa wakipewa asilimia 20 pekee za kubaki kwenye operesheni hiyo ambayo mwisho iliofanikiwa.

Mama mzazi wa watoto hao, Angela Formosa amesema ilikuwa ni kama miaka milioni kuwasubiri watoto wake hao kuweza kutoka kwenye chumba cha upasuaji.

_90964334_twins1pa
Picha ya Rosie na Ruby kabla hawajafanyiwa upasuaji

“Miaka minne iliyopita akilini mwangu sikufikiria kitu kama hiki kingelitokea. Nilipokuwa mjamzito sikudhani nitaiona siku ya ya kwanza shuleni kwa hivyo inanifurahisha sana kwa hiyo nashukuru sana hospitari ya I Gosh [Great Ormond Street Hospital] kwa kweli.”

Formosa alijifungua watoto hao katika hospitali ya Uversity College of London kwa njia ya upasuaji mwaka 2012 huku ujauzito huo ukiwa na takribani wiki 34 na baada ya saa chache kuzaliwa walipelekwa katika hospitali ya Great Ormond Street kwa ajili ya upasuaji huo wa kuwatenganisha.

_90964336_twins2pa
Picha ya Rosie na Ruby walipotimiza mwaka mmoja

Naye Profesa Paolo De Coppi ambaye ni mtaalamu wa upasuaji wa watoto katika hospitali ya Gosh, amesema kuwa ni furaha kwa watoto hao kusikia kuwa wanakaribia kuanza shule.

“Ni furaha wakati wote kushuhudia maendeleo ya wagonjwa na kusikia kwamba wamepiga hatua kimaisha – hii inafanya kazi tunayoifanya kuwa ya kuridhisha,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents