Burudani ya Michezo Live

Mapenzi: Lady Jaydee kuwakonga nyoyo wapendanao (+video)

Mwanamuziki Lady Jaydee anatarajia kukonga nyoyo za mashabiki wake kupitia show yake ya ‘Valentine Day na Lady Jaydee’ ambayo ameandaa kwa ajili ya wapendanao.

Muimbaji huyo amesema si lazima mtu awepo kwenye mahusiano au awe na mwenzake ili aweze kufaidi burudani hiyo ila ni yeyote anaweza kufika Serena Hotel hapo kesho, February 1o kwa ajili ya kusuuza moyo wake.

“Nawakaribisha sana wote waje kujumuika na mimi na ukizingatia mara ya mwisho ku-perform Dar ilikuwa mwaka jana mwezi wa tatu na malalamiko mengi niliyapata kwa watu kwa sababu watu walikuwa wameshazoea kuona Lady Jaydee na Machozi Band kila wiki, amesema na kuongeza.

“Lakini siwezi kuishi maisha hayo hayo kila siku na kwa kuwa hawawezi kupata hiyo nafasi ninapopata nafasi ndio nawatengenezea kitu kama hiki,” Lady Jaydee ameiambia Bongo5.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW