Mapenzi Mazuri Yaleta Ufanisi kazini

Mapenzi Mazuri Yaleta Ufanisi kazini
Kuna mahusiano kati ya ufanisi wako kazini na maisha ya
kimaingiliano kimapenzi (Sex life). Hii ni kwa mujibu wa matokeo ya
tafiti iliyofanywa katika Chuo Kikuu cha Gothenborg nchini Sweden

Tafiti hiyo inabainisha mahusiano mema ya kimapenzi baina ya wawili
wapendanao na maingiliano ya kimapenzi yenye furaha kwa wapendanao
hupelekea kupungua kwa msongo na hata hatari za kuwa na afya mbaya kwa
mtu aliye kazini.

Kinyume chake kwa maana ya mahusiano na maingiliano ya kimapenzi
yasiyoleta furaha hupelekea hali ya msononeko na hata matatizo ya mara
kwa mara ya kukosa usingizi.

Tafiti hiyo inaonyesha pia, kuwa kuridhika kimapenzi hutofautiana
baina ya mwanamke na mwanamme. Kwa wanaume wengi, tendo la ndoa
hupelekea kuridhika kimapenzi. Kwa mwanamke, kuridhika kimapenzi
inaendana na mahusiano mengine ikiwamo kukumbatiana na kuwasiliana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents