Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Mapigo ya Vanessa Mdee jukwaani yambadili Gigy Money

Msanii wa muziki Bongo, Gigy Money ameeleza sababu ni kwanini sasa hivi anajitahidi kupunguza mwili wake.

Muimbaji huyo amesema anahitaji kuwa na mwili ambao utamfanya aweze kutumbuiza vizuri jukwaani kama anavyofanya Vanessa Mdee.

“Kuna muonekano wa show tofauti na picha za Instagram mimi sasa hivi ni performer, huwezi kwenda jukwaani una limwili lako tu. Kwa hiyo mtu unatakiwa na mwili fulani hivi,” amesema.

“Do you look Vanessa akiwa ana-perform, how do you feel unaoana kabisa machachari, anaweza kuwa na bendi, anaweza kuinua mguu, unafurahi, sio mtu shabiki anasubiri utikise makalio tu,” Gigy Money ameiambia Bongo5.

Kabla ya kuingia kwenye muziki Gigy Money alikuwa akitokea kwenye video za wasanii kama video vixen. Kwa sasa ni msanii mwenye nyimbo tatu ambazo ni Supu, Papa na Mimina.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW