Habari

Mapiramidi ya kale yafunguliwa Misri, ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1965

Misri imefungua kwa ajili ya watalii mapiramidi mawili ya kale kusini mwa Cairo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1965 baada ya kuhitimisha shughuli ya ukarabati.

Image result for Pyramids for the First Time Since 1965

Wizara inayoshughulikia mambo ya kale imesema kwenye taarifa yake kwamba waziri wake Khaled al-Anani alifungua piramidi lililoinama la Pharao Snerefu na piramidi inayohusiana na ya kwanza ililopo Dahshur Necropolis mjini Giza.

Al-Anani alinukuliwa akisema kwamba mapiramidi hayo kwa pamoja yameorodheshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO kuwa urithi wa dunia kama sehemu ya makaburi ya kale ya Memphis.

Piramidi hiyo iliyoinama yenye urefu wa mita 101 ni mfano wa kipekee wa mapiramidi ya kwanza yaliyojengwa nchini Misri.

Lilijengwa na Pharaoh Snerefu aliyekuwa mwasisi wa kizazi cha nne cha ufalme wa Misri enzi za ufalme wa zamani miaka 2600 kabla ya Kristo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents