Burudani

Mapokezi ya ‘Boss’ yamduwaza Elly da Bway

Elly da Bway adai ameyashangaa mapokezi aliyoyapata kwenye wimbo wake mpya ‘Boss’.

Mtayarishaji huyo wa muziki na msanii wa Spacious, ameiambia Bongo5, wimbo huo aliuachia kikawaida lakini kilichotokea ni tofauti walivyokuwa wakifikiria hapo awali.

“Ni takriban wiki mbili zimepita sasa tangu nilipoachia wimbo wangu mpya, lakini mapokezi yake ninavyoyaona yamekuwa makubwa tofauti na tulivyofikiria mwanzo na uongozi wangu. Huu umekuwa mwanzo mzuri kwa kuwa ndio wimbo wangu wa kwanza, imeniongezea nguvu ya kufanya kazi nzuri zaidi kwa ajili ya mashabiki wangu,” amesema Elly.

“Tayari nina nyimbo nyingi zipo store, naangalia muda muafaka wa kuachia kwa sasa naipa muda kidogo wimbo huu upite,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents