Burudani

Mapokezi ya Darassa Kenya Ni Moto Wa Kuotea Mbali

Staa wa kibao, Muziki, Shariff Thabit alamaarufu Darassa, kwasasa hashikiki kwa jinsi alivyopanda chati kwa ghafla kwenye muziki wa kizazi kipya Africa. Darassa ambaye kwasasa ameachia kibao kingine kikali pamoja na video yake, amemwaga petroli kwenye moto uwakao. Niajabu kuwa Darassa bila ya kutumia kiki, ameweza kukubalika kirahisi kinyume kabisa na wasanii wengine wakali Africa Mashariki. Kupitia makala haya, nitakupa nafasi ya kubaini mwenyewe ukweli huu wa mambo ambao haufichiki ja kinga cha moto kilicho fichwa chini ya majani yaliyo kauka.

Takribani wiki mbili zilizopita, Darassa akiandamana na Ben Paul na AY ambaye Darassa amenukuliwa kusema yeye ndiye anayempa na kumuonesha njia zakupitia ilikuyafikia malengo yake kimuziki, waliitembelea nchi ya Kenya kwa ajili ya kupiga show mjini Nairobi na pia kufanya media tour yake ya kwanza nchini humu. Na kwakweli kupitia kanda za video ambazo ninakukonyezea hapa chini utakubaliana nami kuwa Darassa yuko katika level nyingine kabisa tofauti na wasanii wengine wa Tanzania na Africa Mashariki kwa jumla. Kati ya vyombo vya habari alivyowahi kuvitembelea, vilikuwemo viwili vikubwa si Kenya pekee bali humu barani Africa nikizungumuzia Citizen TV na NTV. Hebu jionee mapokezi yake kwenye runinga ya Citizen Tv kwenye kipindi maarufu cha burudani cha 10 over 10 kwenye kanda video ya kwanza pengine utaelewa ninini nachokisema.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=umvrrTdwzZk[/embedyt]ye kipindi maarufu cha Burudani #TheTrend, kinacho rushwa hewani kila siku ya Ijumaa na kinacho endeshwa na mtangazji maarufu Larry Madowa. Darassa pia alifunguka na kwa mara ya kwanza wakenya ama mashabiki wake walipata fursa yakujua kuwa Msanii mkali na staa wa Zigo Ambweni Yesaya aka AY pia ni mmoja ya wadau wanao masaidi kuzikwea ngazi za juu kimuziki. Hebu afatilie interview nzima ya Darassa akihojiwa kwenye kipindi cha #TheTrend kwenye runinga ya NTV ili uzidi kupata uhondo zaidi na uelewe kwa kina mktadha wa makala haya maalumu.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=PhX1ZRpDvqk[/embedyt]hi ya Kenya, aliwahi kuwaacha midomo wazi wengi pale alipoangusha burudani la kukata na shoka kwenye show yake nchini Burundi. Chakutia moyo na kufuhisha na kuburudisha zaidi, ni jinsi mashabiki wake wa nchini Burundi walivyoimba nyimbo zake pamoja naye alipokuwa jukwaani na kilichowagusa wengi ni pale mashabiki walivyopagawa na nyimbo ya Muziki pale Dj alipoiachilia hewani. Hiki sikitu cha kwaida, inamaanisha Darassa ameingia kwenye wasanii ”Extra-odinary”. Hebu tupia jicho na hii video ya Darassa akiwa Burundi, alivyojaza ukumbi huku mashabiki wakimshangilia kwa vifijo na nderemo.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=9oahrK2h0Yc[/embedyt]ji chake si cha kupapasa. Maana kibao chake kipya Hasara Roho, alichokiachia wiki iliyopta hakika nakifananisha na bomu la nukilia la Nagasaki kule nchini Japani wakati wavita vya pili vya Dunia. Wakati jeshi la wanahewa la Marekani lilipofanya shambulizi lililoacha maafaa makubwa na madhara ya kiafya ambayo bado yanashudiwa mpaka sasa. Sitaki nikupoteze mwenzangu, ila mashairi ya wimbo Hasara Roho yanaua na kuumiza wasio mpenda na pia kufurahisha na kuburidisha wafuasi wake kwa wakati mmoja. Aisee huyu jamaa kwasasa ni level nyingine, na wala hahitaji kiki kukiki ja mashairi yake ya wimbo Hasara roho yanavyosema. Nikinukuu ” Kama uantaka kiki kwa Pikipiki, mara black mara white vipi, kama unatikisa kibiriti I am play no game am sorry rafiki.” Kweli Darassa si wamuchezomuchezo, na anastahili kongole.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents