Burudani ya Michezo Live

Mapokezi ya wasanii watakaofanya ‘show’ ya Wasafi Festival Kenya usipime (Picha)

Wasanii watakaofanya onesho Jumatato hii katika Tamasha la Wasafi Festival nchini Kenya kutoka Tanzania wamepokewa kwa shangwe kubwa na Wakenya hapo jana.

Awali show hiyo iliingiwa na sitofahamu baada ya msanii Diamond na Rayvanny kutoruhusiwa kufanya onesho nje ya nchi baada ya kufungiwa na BASATA kwa kosa la kuimba wimbo Mwanza ambao ulifungiwa na baraza hilo.

Lakini mapema jana baraza hilo lilitoa ruhusa kwa waimbaji hao ya kufanya enesho kwa madai adhabu ya kufungiwa ilikuja kwa wawili hao wakati tayari wameshaingia makubaliano ya enesho la Kenya.

Baada ya team hiyo kuwasili nchini Kenya, Rais wa WCB Diamond Platnumz aliwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kwaajili ya enesho hilo la aina yake.

“Earlier Today in MOMBASA!!!…. Kesho kwa Pamoja Tunaandika Historia ya #WasafiFestiVal208 kwa Mara ya Kwanza ndani ya Kenya Tena Mjini MOMBASA!!!….. tafadhali nunu ticket yako sasa kupotia Mookh.com au wahi Mapema Getini maana najua kabisa ticket ukichelewa zigakiwa shida….. na usije kulalamika umekosa…. follow @nrgradioke kwa Taarifa zaidi!!!!,” aliandika Diamond.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW