Habari

Maporomoko ya matope yalisababishwa na mvua za masika mashariki mwa Uganda yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 30

Maporomoko ya matope yalisababishwa na mvua za masika mashariki mwa Uganda yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 30

Maporomoko ya matope yalisababishwa na mvua za masika zinazonyesha katika maeneo ya milimani mashariki mwa Uganda yamesababisha msiba mkubwa na hasara ya kuporomoka kwa majumba na daraja katika wilaya ya Bududa.

Watu 34 wamefariki Uganda kufuatia maporomoko ya matope yalisababishwa na mvua za masika zinazonyesha katika maeneo ya milimani mashariki mwa nchi hiyo.Maeneo hayo yanajulikana kwa majanga ya aina hiyo amesema afisa mmoja wa shirika la msalaba mwekundu.

Wahanga zaidi huenda wakagulika wakati timu ya uonkoaji ikiyafikia maeneo yote yaliyoathirika katika maeneo ya chini ya mlima Elgon.Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu Irene Nakasita ameeleza hayo na kufafanua kwamba watu wamefariki kutokana na kuangukiwa na maporomoko na mawe yaliyoporomoka kutoka milimani kufuatia mvua za mfululizo ambazo zimenyesha kwa kipindi kirefu siku ya alhamisi mchana katika wilaya ya Bududa.

Majumba yaliharibiwa katika takriban vijiji vitatu na kuna pia waliopatikana baadhi ya viongo vyao tu kutoka kwenye matope hayo. Shirika hilo la msaada la msalaba mwekundu linasema linatarajia idadi hiyo kuongezeka kutokana na kuwa watu wengi bado hawajapatikana.

Kamishna wa serikali anayehusika na masuala ya usimamizi wa shughuli za kudhibiti majanga katika eneo hilo Martin Owor amesema kuna mto unaopita kwenye eneo hilo ambao ulivunjika  kingo zake na kuharibu daraja na pia kusababisha hatari katika maakaazi ya karibu na hapo.

Mnamo mwezi Machi mwaka 2010 takriban watu 100 walifariki katika tukio kama hilo la maporomoko ya matope katika eneo la Bududa na kila mwaka kunaripotiwa watu kujeruhiwa na kufariki wakati wa msimu wa mvua toka wakati huo. Owor amefahamisha kwamba mpaka wakati huu tayari maiti za watu 31 zimeshapatikana na kutambuliwa kufuatia janga hili.

Ikumbukwe pia kwamba juhudi za serikali ya Uganda katika kipindi cha miaka kadhaa za kujaribu kuwahamisha wakaazi kutoka maeneo hayo ya chini ya milima hazijafanikiwa.Kadhalika imekuweko miito inayotolewa ya kuwataka watu wapande miti mingi zaidi katika maeneo hayo ya milimani.

Chanzo DW Swahili

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents