Soka saa 24!

Mapromota feki wamzingua Sharomilionea

 

Video_sharo_hammer
Mwigizaji na mwimbaji ambaye amegundua staili ya kutembea kisharobaro, Sharomilionea hivi juzi amewalalamikia Promota Mwasiti kutoka Iringa kwa kitendo chake cha kutumia uwezo wake wa kifedha, na kutumia fedha kama fimbo kwa kuwachapia wanyonge.

 

video_sharo_milionea_na_madem

 

Anasema mwanamama huyo alimwita yeye akiwa na wasanii wengine kwaajili ya kufanya show tano, lakini baadaye akaghaili na kuwaambia watafanya shoo mbili Iringa na Simbawanga.

anasema baada ya makubaliano hayo akapiga show ya kwanza Iringa, ambayo ilikuwa mzuri na kulipwa chake mapema hata kabla show haijaisha, na baadaye ikafuata ya Simbawanga ambayo nayo alimaliza salama.

Sharomilionea anasema katika show hiyo ya pili  hakumpa fedha zake mpaka alipomaliza, ambapo alipozipata alimuomba amkatie tiketi kwaajili ya kurudi kuendelea na filamu kwakuwa tayari alikuwa akisubiliwa na King Majuto, Dude na Steven Nyerere.

Anasema mama huyo akaanza kumlazimisha  afanye show nyingine asubuhi ya bule kwakuwa watoto wanampenda sana, hivyo watatozwa buku buku jambo ambalo Sharo anasema hakukubaliana nalo.

anasema kwa kuwa alikuwa na mikakati mingine, alimuomba mwanamama huyo akamkatie tikati yake haweze kurudi, lakini alijibiwa kwamba tiketi zimeisha. Sharo anasema ikabidi atoe fedha zake na kwenda kukata tiketi mwenyewe na kuondoka hapo kwakuwa alijua tayari imeshakuwa balaa.

Anasema wakati anaondoka  ndipo akapigiwa siku kwamba yule mama amepanga kutumia fedha zake kwaajili ya kumchafua, kwenye stesheni mbalimbali za redio zinazozunguka mikoa ya hapo karibuni.

anasema alijaribu kuongea na huyo mama Mwasiti, lakini aliambiwa asuburi kwani atamfanyizia kwakuwa yeye aliamua kumdhalilisha kwa show aliyoiandaa.

Sharo anasema aliamua kupiga simu kwa wasanii wenzake na kuwahadithia lakini walimwambia aachane naye. pia anasema akapata simu kutoka kwa mapresenter wa stesheni hizo za redio, na kumwambia wamepata taarifa hizo kwamba wasipige nyimbo zake lakini wamechunguza na kuona hakuna tatizo.

lakini huyo mama hadi sasa bado hajachoka analengo la kumuharibia kwa wanajamii ili   Sharo akiitisha tamasha mikoa hiyo kusiwe na watu………

Na hayo ndiyo matatizo ya mapromota wa kibongo bongo……………..

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW