Michezo

Mapya yaibuka kikao cha Mourinho na bosi wa United, Zlatan kurudishwa

Mapya yameonekana kuibuka baada ya kikao cha faragha baina ya mkurugenzi wa klabu ya Manchester United, Ed Woodward dhidi ya Jose Mourinho kilichofanyika hapo jana siku ya Alhamisi.

Kikao hicho kilichotangazwa siku mbili zilizopita kuwa wawili hao wangekutana ndani ya saa 48 zijazo na kujua hatma ya klabu hiyo ambayo imeonekana kutoanza vyema msimu huu huku wengi wakifikiria kutakuwana maamuzi magumu ya kutimuliwa kwa kocha Jose Mourinho imeonekana kuwa ni tofauti na matarjio ya wengi.

Mbivu na mbichi kuhusu Jose Mourinho kujulikana saa 48 zijazo

Licha ya kutojua hasa kilichoendelea ndani ya kikao hicho kwakua Mreno huyo bado anaendelea na majukumu yake kama kawaida ila tofauti na matarajio ya wengi, Mourinho amehitaji kumrudisha aliyekuwa mshambuliaji wa Man United, Zlatan Ibrahimovic kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari.

Zilatan mwenye umri wa miaka 37, ameondoka klabuni hapo na kujiunga na timu ya LA Galaxy ya nchini Marekani mwezi Machi baada ya kushindwa kukisaidia kikosi cha Mreno huyo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Mchezaji huyo ameonekana kuwa na uwezakano mkubwa wa kurudi baada ya Paul Pogba na Alexis Sanchez kuonekana kutokidhi kwenye nafasi za uongozi ndani ya timu hiyo.

Wakati hayo yakiendelea ripoti zinasema kuwa aliyekuwa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger hakukubaliana na kitendo cha watu kuhitaji Alexis Sanchez kujiunga na United,

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile alitua United dirisha la usajili wa Januari akipishana na Henrikh Mkhitaryan.

Huku ripoti hiyo ikienda mbali zaidi na kusema kuwa Wenger alikuwa kinyume na wachezaji wote waliyotaka kwenda kujiunga na meneja Mourinho.

Michezo mitano ijayo atakayocheza Manchester United ni Oktoba 20 dhidi ya Chelsea, Juventus (Oktoba 23), Everton (Oktoba 28), Bournemouth (Novemba 3) na Juventus (Novemba 7)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents