Burudani

Mara ya kwanza nilikutana na Vanessa Mdee studio – Brian

Msanii wa Bongo Flava na wa pili kusainiwa chini ya Mdee Music, Brian ameeleza namna alivyokutana na Vanessa Mdee hadi akapata nafasi ya kuwa chini ya label hiyo.

Brian ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Gambe’, ameiambia Daladala Beats ya Magic Fm kuwa alikutana na Vanessa studio kwa Nahreel (The Industry).

“Actual mara ya kwanza ninakutana na Vanessa nilikuwa kwenye studio ya Nahreel na aliniite yeye, actual yeye ndiye alinipigia simu akaniambia njoo tuongee, and so exited kwanza unaingaia kwenye chumba hapa kuna Nahreel, Aika naVanessa.

“Lakini nilipenda sana tulivyozungumza kwa kuwa kulikuwa hakuna ile super star element ambayo ma-super star wengi wanayofanya, aliongea na mimi kama another musician sio kama mtu amenizidi na ndicho nilipenda zaidi na ndio one of reason niliamua ku-join,” amesema  Brian.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents