Michezo

Maradona atolea macho Aston Villa

 

Aliyekuwa kocha wa Argentina, Diego Maradona amesema anataka kuinoa Aston Villa


ambayo iko mbioni kumtafuta kocha mpya. Mkongwe huyo amesema anataka kufundisha soka katika ligi kuu ya England kwa madai ligi hiyo ni nzuri na vyombo vya habari vinaheshimu uhuru binafsi. Maradona ameweka wazi tamanio lake kuchukua nafasi ya kocha Martini O’Neill aliyetimka Aston Villa.

Msemaji wa Maradona amesema iwapo Aston Villa watamfuata kocha huyo basi atapokea ofa kwa mikono miwili kwani anasubiri kwa hamu.

O’Neill aliacha kibarua wiki mbili zilizopita na sasa Kevin McDonald anainoa timu hiyo kwa muda. Jambo zuri nikwamba ameisaidia timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Ham katika mchezo wa ligi kuu England mwishoni mwa wiki hii.

Kocha wa Ajax Martin Jol na kocha wa Marekani Bob Bradley ni miongini mwa watu wanaopewa nafasi kubwa ya kuinoa timu hiyo.

Mwakilishi wa Maradona amesema ni vizuri kama Aston Villa itamnasa kocha huyo ambaye alitoamsisimuko katika fainali za kombe la Dunia katika mechi za awali kabla ya kufungwa na Ujerumani 4-0 katika hatua ya robo fainali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents