Michezo

Maradona amkubali mwanae wa nje Diego Junior

Mchezaji nguli wa soka wa Argentina, Diego Maradona hatimaye amemkubali mtoto wake Diego Junior aliyekuwa naye mwishoni mwa wiki iliyopita huko Buenos Aires.

_90971510_maradona-

Diego Junior alizaliwa nchini Italia mwaka 1986 kutoka katika mahusiano ya pembeni aliyokuwa nayo lakini hakuwahi kukubalika rasmi na baba yake, hata baada ya kulazimishwa kuwa analipa fedha za matumizi na jaji wa Italia mwaka 1992.

Maradona mwenye umri wa miaka 55, sasa amemkubali rasmi mtoto wake huyo na kudai mbele ya wanahabari kuwa huyo ni mtoto wake wa kiume. Maradona pia aliendelea kudai kuwa anadhani Diego Junior anafanana na baba yake pamoja na kukataa kufanya vipimo vya DNA kwa miaka kadhaa kufuatia kutakiwa kufanya hivyo na mahakama.

Naye Diego Junior aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa amefurahi hatimaye kukubaliwa na baba yake kwani walisubiria hilo kwa kipindi cha miaka 30.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents