Tupo Nawe

Marafiki wamtaka Pochettino kuachana na Arsenal, Madrid ili muandalia mkwanja Mourinho aachane na Spurs asubiri Zidane atimuliwe 

Marafiki wa karibu wa Kocha aliyetimuliwa kazi ndani ya klabu ya Tottenham, Pochettino wamemshauri kutokimbilia kazi ya usimamizi katika timu ya Arsenal wakiamini anaweza kupata kazi nzuri zaidi. (Sunday Telegraph)

Pochettino ameshauriwa kutokimbilia kazi ya usimamizi katika klabu ya Arsenal na marafiki zake ambao wanaamini anaweza kupata kazi nzuri zaidi

Watford imeitisha mkutano siku ya Jumapili ambao unadaiwa ajenda yake itakuwa kumfuta kazi Quique Sanchez Flores kwa mara ya pili. (The Athletic – subscription required)

Arsenal huenda ikasubiri hadi msimu ujao kumsajili mkufunzi Brendan Rodgers, lakini kocha huyo wa Leicester anachukulia nafasi ya Gunners kama kazi ya ndoto yake. (Star on Sunday)Mkufunzi wa Leicester, Brendan Rodgers

Haki Arsenal huenda ikasubiri hadi msimu ujao kumsajili mkufunzi wa Leicester, Brendan Rodgers

Naibu mkufunzi wa Manchester City, Mikel Arteta ni mtu ambaye Arsenal inamtaka kuchukua nafasi ya Unai Emery. (Sunday Mirror)

West Ham inamfuatilia mkufunzi wamuda wa Arsenal, Freddie Ljungberg kama mrithi anayepigiwa upatu kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini. (Star on Sunday)

Jose Mourinho alipewa ofa ya pauni milioni 12 na Real Madrid kutochukua kazi nyingine ya ukufunzi ili asubiri Zinedine Zidane afutwe kazi kabla ya kujiunga na Tottenham. (Sun on Sunday)Jose Mourinho

Kabla ya kujiunga na Tottenham, Jose Mourinho alipewa ofa ya £12m na Real Madrid kutochukua kazi nyingine ya ukufunzi ili asubiri Zinedine Zidane afutwe kazi

Everton inamtaka kocha wa Bournemouth, Eddie Howe, ambaye ni shabiki wa zamani wa klabu hiyo zama za ujana wake, kumrithi meneja Marco Silva anayekabiliwa na wakati hatari ya kufutwa katika klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Real Madrid inapanga kuweka dau la £70m kumnunua mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, huku kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez, 28, iikijumuishwa katika mpango huo. (Eldesmarque, via Star)

Chelsea inamfuatilia kwa karibu mchezaji Zaha na winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19, inapojiandaa kuimarisha safy yake ya mashambulilizi. (Sunday Express)Pierre-Emerick Aubameyang

Real Madrid inapanga kuweka dau la £70m kumnunua mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30,

Mshambuliaji wa Uhispania wa miaka 31-Diego Costa, ambaye alijiunga na Atletico Madrid kutoka Chelsea mwaka 2018, anatarajiwa kujiunhga na Flamengo kwa mkataba wa £25m. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Liverpool na Tottenham wako tayari kumenyana katika kinyang’anyiro cha usajili wa mchezaji wa safu ya kati ya Lyon na Holland, Memphis Depay, 25. (Sunday Express)

Paris St-Germain bado haijampatia mkataba mpya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20. (Le10Sport – in French)Kylian Mbappé

Paris St-Germain bado haijampatia mkataba mpya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe

Manchester City inamnyatia beki wa Leicester na Uturuki, Caglar Soyuncu, 23. (Sunday Times – subscription required)

Kipa wa England, Jordan Pickford, 25, anasisitiza kuw awachezaji wa Everton wanamuunga mkono mkufunzi wao Marco Silva na kwamba hawako tayari kumuona akifutwa kazi. (Observer)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na West Ham, Javier Hernandez yuko tayari kuhamia MLS. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico wa miaka 31, alijiunga na Sevilla mwezi Septemba. (LA Times)Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na West Ham, Javier Hernandez yuko tayari kuhamia MLS

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na West Ham, Javier Hernandez yuko tayari kuhamia MLS

Aston Villa wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Ivory Coast, Jonathan Kodjia, 30, mwezi Januari. (Football Insider)

Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasubiri kufunguliwa tena kwa dirisha la uhamisho wa wachezaji kumnunua mshambuliaji Wilfried Zaha, 27. (London Evening Standard)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW