Marais Wastaafu Kikwete na Mkapa watoa kauli kwenye msiba wa Rais Mstaafu wa Kenya, Moi

Marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete baada ya kutua Jijini Nairobi kwa ajili ya mazishi rasmi ya Rais mstaafu wa Kenya, Hayati Daniel arap Moi, walipata wasaa wakutoa salamu za rambimbali.

 

Rais Mstaafu Kikwete wakati akizungumza kutoa heshima za mwisho, kwa Rais Mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi, katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo mjini Nairobi, alisema “Tupo pamoja nanyi, niko pamoja nanyi, msiba wenu ni wangu, msiba wenu ni wetu, uchungu wenu ni wangu, uchungu wenu ni wetu, maombolezo yenu ni yangu na ni maombolezo yetu sisi wote”

 

Naye Rais Mstaafu Mkapa alisema”Nilikuwa Rais wa Tanzania miaka kumi. Katika miaka hiyo kumi, miaka saba nilikuwa nafanya kazi na Rais Moi.
Pamoja na kwamba ni mzee wetu, lakini kwangu mimi alikuwa ‘mentor’ wangu katika utawala na uongozi.  Ndio sababu nilisema lazima nije na ku ‘pay last tribute’ (kutoa heshima za mwisho) kwa uhusiano huo niliokuwa nao, lakini vilevile kushirikiana nanyi katika kumuombea, apumzike mahali pema peponi, kwa Mungu wetu ambaye alimpenda sana,”

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW