Habari

Marapper wakongwe wajitokeza kumpa shavu Lil Kim

Female rappers wakongwe kwenye game ya Hip Hop wa long time, Eve, Missy Elliot na Pepa kutoka kundi la Salt and Pepa na wengine wengi walijitokeza kumpa shavu shoga yao Lil Kim kwenye show aliyopiga New York City wikiendi iliyopita.

Mafans wa Kim wamefurahishwa na kitendo cha msanii huyo kurudi kwenye rap game kwa kishindo baada ya miaka michache kuwepo kimya kutokana na matatizo ya kufungwa jela na baadaye uhusiano wake wa kimapenzi na peoducer Scottt Storch kuharibika.

Kim alirudi kwenye game akijaribu kuclaim taji lake la zamani la ‘The Greatest female rapper alive’, ila akakuta mwanamama Nicki Minaj akiwa amekalia nafasi hiyo na kuiga yale ambayo kim alikua anafanya enzi zake akiwa kileleni mwa shughuli za rap.
Kim alilianzisha beef na Minaj ambalo limezua gumzo kubwa kwenye tasnia ya Hip Hop duniani kote huku wawili hao wakizungumziana kwenye vyombo vya habari na kutoa freestyles dhidi yao wenyewe kwa wenyewe.
Fans wa Kim wamesema enough with the beef! Sasa akomae kutoa album na miziki itakayodhibitisha yeye ni mkali kama yule wa enzi zile.

Lil Kim anatarajia kufaya tour kweney sehemu mbalimbali nchini Marekani itakayoitwa ‘Return of the queen’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents