Burudani

Marco Chali: P-Funk alikosea kumuachia Lamar aondoke Bongo Records

Mtayarishaji wa muziki wa MJ Records, Marco Chali amesema kama P-Funk Majani angemwacha Lamar aendelee kukaa Bongo Records, umaarufu wa studio hiyo usingeshuka kama sasa.

1517242_434330776709684_1387853801_n

Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi hivi karibuni, Marco alisema huenda kushuka kwa Bongo Records kulitokana na P-Funk kuchoka kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu.

“MJ alivyoona ‘bana mimi huu muziki basi’ akaona kuna mishale ipo, sasa unanunua ule mshale una umiliki ili upige kule kule lakini ukiwa pembeni, ambapo P-Funk kama angemchukua Lamar akakaa naye Bongo Records, labda ingekuwepo mpaka sasa hivi tena ikiwa active,” alisema Marco Chali.

“Sasa alimruhusu aende. Kwahiyo ni hivyo, ni trick ya kujua mimi labda nimechoka, Majani unajua kafanya kazi nyingi sana, kwahiyo labda imefikia kipindi labda na yeye apumzike, lakini studio ili iendelee kuishi anaweka mtu mpya,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents