Marco Reus ajifunga kitanzi Dortmund mpaka 2023

Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Borussia Dortmund ya Ujerumani, Marco Reus amesaini mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kuichezea timu hiyo.

Reus amesaini mkataba huo ambao utamfanya kuendelea kubakia Dortmund mpaka ifikapo mwaka 2023.

Mchezaji huyo amekuwa nje ya uwanja kwa takriban miezi nane kutokana na kuuguza majeraha ya goti.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW