Michezo

Marcus Rashford ni kipaji maalum – Louis van Gaal

Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 18, Marcus Rashford ni kipaji maalum, kwa mujibu wa kocha wa Manchester United, Louis van Gaal.

3191574800000578-0-image-m-28_1456487734530

Kijana huyo amecheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza kwa kufunga magoli mawili kwenye mchezo dhidi ya Arsenal uliomalizika kwa mabao 3-2.

Rashford alifunga mabao mawili kwenye mchezo wake wa kwanza na timu hiyo dhidi ya FC Midtjylland kwenye Europa League Alhamis hii.

Van Gaal alisema: Chipukizi mara nyingi hucheza vizuri kwenye mechi ya kwanza. Ya pili ni tofauti. Marcus alicheza vizuri kwenye yote miwili hivyo ni kipaji maalum.

31A626D400000578-3469105-image-a-45_1456744544124

Kocha huyo wa zamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich amesema mwanzo wa Rashford unafananishwa na ule wa mastaa wakubwa kwenye soka kama Patrick Kluivert, Xavi na Thomas Muller.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger naye amedai kufurahishwa na uwezo wa kinda huyo.

31944F3C00000578-3465477-image-m-41_1456488458328

Kabla ya mechi hizo, Rashford alikuwa mchezaji wa benchi ambaye hakutumia kwenye mchezo wa timu yake na Watford November 21 na kwenye sare na Leicester wikiendi iliyofuatia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents