Habari

Marehemu Mh. Elly Macha aagwa rasmi

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa pamoja na wabunge mbalimbali wameshiriki kuuaga mwili wa aliyekua mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt Elly Macha, aliyefariki nchini Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili huo umewasili alfajiri leo, katika uwanja wa Mwalimu Nyerere ambapo mapokezi yaliongozwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson na kusafirishwa tena mpaka Dodoma ambapo viongozi wa bunge wamepata fursa ya kuuaga Mheshimiwa Macha kwenye viwanja hivyo vya bunge.

Dkt Macha alifariki dunia Machi 31 mwaka huu katika hospitali ya New Cross, Wolverhampton iliyopo nchini Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu.

Aidha Naibu spika, Dk Tulia Ackson amesema Bunge lilipata taarifa za ugonjwa wa marehemu ndani ya miezi mitatu na baadae kupata taarifa juu ya kifo chake na kusema kwamba, licha ya kua na ulemavu, Dkt Macha alipigania haki za walemavu kijasiri na kikamilifu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents