Habari

Marekani: Afisa ngazi ya juu Urusi aliamuru kiongozi wa upinzani kupewa sumu 

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo amesema kuwa inawezekana kitendo cha kumpa sumu kiongozi wa upinzani nchini Urusi, Alexei Navalny kiliamuliwa na afisa wa ngazi ya juu wa serikali ya Urusi.

Pompeo calls Alexei Navalny poisoning 'abhorrent attack to justice'

Pompeo amejizuia kutoa maelezo zaidi kuhusu hoja hiyo, akiongeza tu kuwa watu wote duniani wanatambua kilichotokea.

Akizungumza katika mahojiano na chombo kimoja cha habari cha Marekani, Waziri Pompeo amesema kuwa serikali ya Marekani itatafakari cha kufanya kujibu kisa hicho cha kumpa sumu Navalny, kwa lengo la kuhakikisha kuwa vitendo kama hivyo havitokei tena.

Alexei Navalny: Substantial chance Russia behind poisoning, Pompeo says -  BBC News

Wakati huo huo, Ujerumani imekabidhi ushahidi wake kwa shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya silaha za kemikali-OPCW, kuthibitisha kuwa Navalny alipewa sumu aina ya Novichok.

Naye Waziri Mkuu wa Italia, Giussepe Conte amenukuliwa akisema amearifiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin, kuwa ameunda tume ya kuchunguza kisa cha Navalny kupewa sumu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents