Habari

Marekani: Asakwa na Polisi kwa tuhuma za wizi wa zawadi harusini, donge nono kutolewa kwa atakaye toa taarifa zake 

Polisi wanamsaka mwanamke ambae amepachikwa jina la “mvamizi wa harusi ” ambaye amekuwa akishutumiwa kuiba zawadi kutoka kwenye harusi kadhaa kusini mwa jimbo Texas nchini Marekani.

Mwanamke huyo anadaiwa kuiba zawadi za thamani ya maelfu ya dola na pesa kutoka kwa wanandoa wapya wanaooana

Mwanamke huyo ambaye hajatambuliwa amekuwa akishutumiwa kujitokeza kwenye harusi, bila mwaliko, walau katika harusi nne tangu mwezi Disemba.

Polisi pia wameushirikisha umma picha ya mwnamke huyo akiwa dukani akijaribu kutumia kadi ya zawadi ambayo awali ilitumiwa na wanandoa waliofanya harusi karibuni.

Zawadi ya dola 4,000 sawa na zaidi ya milioni Tisa za Kitanzania, (pauni 3,300) imetangazwa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwake.

“Tusiache aharibu siku maalum ya mtu yeyote na tumlete mvamizi huyu wa harusi za watu mbele ya sheria ,” imesema taarifa ya ofisi ya mkuu wa polisi wa kaunti ya Comal – Texas.

Bodi ya maandalizi ya harusi katika eneo hilo imekiambia kituo cha habari cha CBS kuwa inatambua sura za watu waliopiga picha za harusi

“Tumekuwa na harusi za wazi msimu huu wa majira ya joto ambao tumewaona wakizurura wakitafuta watu wanaouza bidhaa na kumbi za haruri,” amesema Rhonda Hollon, rais wa kampuni wa kampuni ya maandalizi ya harusi ya – New Braunfels Wedding Chamber.

https://www.facebook.com/ComalCountyCrimeStoppers/posts/2237424069688837

Bwana mmoja na mkewe waliliambia shirika la habari la NBC kuwa waligundua kwa mara ya kwaza kuwa wameibiwa zawadi wakati walipokuwa katika fungate yao .

“Ninafikiri tulipogundua kwa mara ya kwanza , lilikuwa ni jambo la kusikitisha , lililotufanya tufikirie kwamba hili limetokea,” alisema rittany Flores.

Yeye na mumewe Andy wanasema pia walimtambua mwizi huyo, na wanaamini aliibamamia ya dola fedha taslimu na maelfu ya hundi za dola na kadi za zawadi.

Lakini wanandoa hao wanasema wanatumaini polisi wataweza kumpata muhusika wa uhalifu huoculprit.

“ninafikiri hilo ndilo tunalobaki nalo kutokana na hili, sio kuchacha tu yaishie hapa … Mvamizi wa harusi, kwa jina lolote wanalomuita, muondoshe katika siku yetu ,” alisema Bi Flores. “hawezi kuiba penzi letu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents