Soka saa 24!

Marekani: Boeing 737 Max 8 ni salama

Utawala wa Mamlaka ya safari za anga la Marekani wameziambia kampuni za ndege kuwa wanaamini ndege za Boeing 737 Max 8 zinafaa ,baada ya ajali mbili zilizosbabisha vifokatika kipindi cha miezi takriban sita.

Taarifa hiyo iliyotolewa Jumanne hii ikiwa ni siku 2 toka ajali itokee, imeeleza namna ndege hiyo inavyofaa, ikisema ni salama kupaa.

Shirika la ndege la Singapore limesitisha kwa muda safari za ndege za Boeing 737 Max 8 zinazoingia na kutoka ndani ya nchi hiyo.

Uamuzi huo umetolewa baada ya ndege ya kampuni ya ndege ya Ethiopia aina ya Boeing Max 8 kuanguka Jumapili, na kuwauwa watu 157 waliokuwemo.

Ilikuwa ni ajali ya pili iliyohusisha ndege ya aina hiyo katika kipindi cha chini ya miezi mitano iliyopita.

Uwanja wa Changi nchini Singapore ni wa tano wenye kuwa na shughuli nyingi zaidi duniani na kiituo kinachounganisha safari nyingi za kutoka bara Asia hadi Ulaya na Marekani.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW