Habari

MAREKANI: Dhoruba kali ikiambatana na mvua yapelekea zaidi watu 55,000 kukaa gizani (+Video)

Dhoruba ya kitropiki imesababisha zaidi ya watu nusu milioni wa Marekani kukosa umeme wakati mvua kubwa ikinyesha na dhoruba kubwa ikipiga katika fukwe za pwani ya Ghuba ya Marekani.

Upepo ulipungua baada ya kimbunga kufika sehemu ya pili, siku ya Jumatano lakini dhoruba kubwa iliendelea kupiga katika jimbo la Florida na Alabama.

Mafuriko yamesababisha uharibifu mkubwa.

Pensacola, iliyopo Florida, imeathirika vibaya na dhoruba hiyo imesababisha daraja kuanguka.

“Mafuriko yanaendelea kuwa tishio kubwa la maisha ya wakazi wa Florida Panhandle na kusini mwa Alabama,” kituo cha taifa cha kutathimini mwenendo wa kimbunga kimesema .

Dhoruba hiyo ilisababisha “mvua za miezi minne kunyesha ndani ya saa nne” mjini, chifu wa Pensacola Ginny Cranor ameiambia CNN.

Kimbunga cha Sally kilipiga katika ghuba ya pwani ya , Alabama, majira ya saa kumi na moja kasoro katika saa za huko kwa upepo wenye kasi ya 105mph (169 km/h).

Dhoruba hiyo ilisababisha "mvua za miezi minne kunyesha ndani ya saa nne"

Dhoruba hiyo baadae upepo ulipungua kwa kiwango cha kasi ya 35mph, lakini mvua kubwa imekuwa ikinyesha na dhoruba kubwa kusababisha uharibu mkubwa.

Dhoruba ilitoka kutoka kaskazini mwa fukwe mpaka kwenye makazi 550,000 ambako kulibaki giza Jumatano , vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Kimbunga cha Sally ni miongoni mwa dhoruba zilizopiga katika bahari ya Atlantiki, ambapo maofisa wamedai kuwa wanakaribia mwisho wa orodha ya herufi.

Uharibifu uliotokea sasa?

Mvua haijapimwa inchi katika baadhi ya maeneo lakini kwingine kulirekodiwa kupiga kwa sentimita 45 katika maeneo mengi.

Mafuriko yalifikia futi tano katikati ya Pensacola. Dhoruba hii ni ya tatu kwa ukubwa kuwahi kupiga katika mji huo. Polisi wamewataka watu kutotoka nje kuangalia uharibifu uliotokea kwa kuwa wanachelewesha kazi yao, alisema: “Inapunguza kasi ya utendaji wetu, tafadhari baki nyumbani!”

Upepo wa dhoruba hii haukuwa na nguvu kubwa ya kustaajabisha kama wakati wa kimbunga cha Laura ambacho kilitokea mwezi uliopita.

Mkuu wa kitengo cha polisi cha Escambia amesema hawatarajii uharibifu wa aina hii kutoka kwa kimbunga Sally.

Cavin Hollyhand, mwenye umri wa miaka 50, anayeishi katika maeneo ya pembezoni huko Alabama, ameiambia Reuters: “Mvua ndio inafanya hili kuepo:Si uhalisia.”

Bado kuna wasiwasi wa kuwa na mafuriko makubwa na kuhatarisha maisha ya watu huko Florida-na mpaka wa Alabama, kitengo cha taifa cha kimbunga kimesema .

Gavana wa Alabama Kay Ivey amesema maeneo mengi ya barabarani watayaona na mafuriko makubwa ya kiwango cha kihistoria na kutaka watu kuchukua tahadhari kwa kuzingatia maonyo yatakayotolewa.

Mvua ilionekana kunyesha katika upande wa Alabama, kusababisha barabara kuharibika

Eneo la hifadhi lililopo Alabama limeharibika kwa kiasi kikubwa

Umeme ulikatika kwa wateja 290,000, walibaki bila umeme katika eneo la Alabama na 253,000 katika eneo la Florida.

Nguzo za umeme zilianguka na miti mingi iling’olewa na mvua hizo.

Mvua ilionekana kunyesha katika upande wa Alabama, kusababisha barabara kuharibika wakati dhoruba likipiga katika maeneo ya fukwe.

Maeneo mengine ya ufukweni yaliathirika pia,maeneo ya fukwe yalijaa maji huko Mississippi na mali za watu wa Louisiana zilifunikwa na maji.

Alabama, Florida na Mississippi yametangaza hali ya dharura kutokana na dhoruba hilo.

Kwanini kasi ni ndogo na nini kinafuata?

John De Block, kutoka huduma ya hali ya hewa ya taifa mjini Birmingham, Alabama, aliiambia ‘New York Times’ kuwa kimbunga cha Sally kilikuwa kinatembea kama kasi ya mtoto katika duka la pipi”.

Kimbunga cha Sally kinahusishwa na mabadiliko ya tabia nchi kwa mujibu wa wataalamu.

Utafiti wa mwaka 2018 katika jarida la ‘Nature magazine’ lilibaini kuwa kasi ya kimbunga na dhoruba ya kitropiki inaondoka katika eneo kwa kupungua kwa asilimia 10% kati ya mwaka 1949 na 2016, hali hiyo inasababisha ongezeko la mvua.

“Sally ina tabia ambayo huwa haionekani mara nyingi na hivyo kusababisha kupunguza kasi na mafuriko kuongezeka,” Mkurugenzi wa kitengo cha taifa cha kimbunga Ed Rappaport ameiambaia Associated Press.

Hata hivyo kimbunga Sally, huwa ina vimbunga vingine vinne vya kitropiki – Paulette, Rene, Teddy na Vicky – vinavyopiga kuzunguka bahari ya Atlantiki.

Kama dhoruba jingine moja litapewa jina rasmi – basi Wilfred litakuwa limechaguliwa tayari – mamlaka ya hali ya hewa huwa inachagua majina kabla katika mwaka mzima na wataanza kutoa majina ya dhoruba kwa kutumia herufi za kigiri.

https://www.instagram.com/tv/CFPB-FWAmvd/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents