Habari

MAREKANI: Elicopter yaanguka juu ya jumba la ghorofa 54

Rubani mmoja amefariki dunia baada ya kutua ghafla helikopta juu ya jumba la ghorofa 54 mjini Manhattan.

Helikopta hiyo ililipuka na kushika moto ilipogonga kituo cha AXA Equitable, na hakuna majeruhi mengine yalioripotiwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Rubani ametambuliwa kama Tim McCormack, huku uchunguzi ukianza kufanywa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

 

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema jumba hilo lilitetemeka ndege ilipoanguka juu yake hali ambayo iliwakumbusha wakazi wengi mashambulio ya kigaidi ya Septemba mwaka 2001.

Maafisa hata hivyo wamefutilia hofu kuwa huenda ajali hiyo ni imetokana na tukio la kigaidi.

Ajali hiyo ilitokea vipi?

Ajali hiyo ilitokea nyakati za mchana wakati wa mchana katika barabara ya 787, kaskazini mwa ukumbi wa Times Square.

Ndege hiyo ya injini mbili chapa Agusta A109E, iliyokuwa na rubani pekee yake, ilikuwa safarini kutoka Manhattan kuelekea uwanja wa ndege wa Linden mjini New Jersey.Mabaki ya ndege hiyo juu ya paa la ghorofaMabaki ya ndege hiyo juu ya paa la ghorofa

Lakini dakika 11 baada ya kuanza safari ilianguka juu ya jumba la ghorofa 54, katika kile kinaelezewa kuwa kutua kwa dharura.

Meya wa jiji la New York City Bill de Blasio amesema helikopta hiyo “imeharibiwa kabisa… kutokana na jinsi ilivyogonga chini kwa nguvu”.

Maafisa wa kitaifa wa usalama wa angani wanachunguza kwanini helikopta hiyo ambayo ilikuwa katika safari ya hali ya juu iliamua kusafiri wakati wa hali mba ya hewa .

Bw. De Blasio amesema hajali hiyo haikuwa “hali ya kawaida “, na kuongeza kuwa helikopta hiyo ilihitaji kibali maalum kutoka uwanja wa LaGuardia mjini New York City.

Mamlaka ya usimamizi wa angani zinasema kuwa walekezi wao walihindwa kudhibiti ndege hiyo.

Jengo hilo liko nusu maili kutoka Jumba la Trump Tower, na usafiri wa anga katika maeneo hayo umedhibitiwa kwasababu jengo hilo linamilikiwa na Donald Trump ambeye sasa ni rais wa Marekani.

Watu wanasemaje?

Gavana wa jimbo la New York, Andrew Cuomoamesema: “Ikiwa wewe ni mkazi wa New York, bila shaka uliathiriwa na shambulio la kigaidi la Septemba 9/11. Ajali hii imetukumbusha shambulio hilo.

“Kwa hivyo niliposikia helikopta imegonga jengo mawazo yangu yalielekezwa kwa mawazo ya kila makazi wa New York.”map showing where AXA Equitable building isPresentational white space

Rais Trump amesema ajali hiyo ni “mkasa mkubwa” na ni tukio la ”kusikitisha”.

Nicolas Estevez mmoja wa watu walioshuhudia ajali hiyo aliliambia shirika la habari la Reuters: kuwa “nilisikia mlipuko na mosho mkubwa ukifuka” hali iliyomkumbush shambulio la Semptemba 2011 (9/11).

Kipande cha chuma cha ukibwa wa (30cm) kilianguka barazani mita chache kutoka hapa, alisema

Michaela Dudley, wa Hoboken, New Jersey, ambaye anafanya kazi katika jengo hilo , anasema alihisi kama ni “matetemeko madogo ya ardhi”.Mabaki ya ndege hiyo juu ya jumba la ghorofaMabaki ya ndege hiyo juu ya jumba la ghorofa

“Nilianza kusikia milio ya magari ya zima moto na hapo nikajua kitu kibaya kimetokea,”alisema wakili huyo wa miaka 30.

“Kulikua na tangazo la kutuagiza tutoke ndani ya jengo hilo. Na bila kupoteza wakati nilifungasha virago vyangu , nikachukua simu na kutoka. Eneo la ngazi lilikua limejaa watu waliokua waking’ang’ana kutoka. Tulikua na wasiwasi kwasababu hatukua na ufahamu ni nini kimetokea na watu walikuwa wamejawa na hofu.”

Rubabui alikua nani?

Tim McCormack alitajwa kuwa mtu mwenye ujuzi mkubwa na rubani mkongwa ambaye pia alikuwa afisa wazima moto wa kujitolea.

Shirika la habari la ABC lilitangaza taarifa iliyokua imetolewa na familia ya McCormack, iliyosema: “Familia yetu leo imempoteza mtu wa maana sana, leo ndugu yetu amefariki dunia akifanya kazi aliyoipenda na kutekeleza kwa uadilifu mkubwa.

Ilisema kuwa alitua ghafla juu ya baa la ghorofa “ili asisababishe maafa ya watu wengine bali yake mwenyewe. Ndugu yangu alikuwa shujaa”.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa Bw. McCormack aliwahi kutua helikopta salama baada ya ndege kukwama ndani ya injini mwaka 2014.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents