Habari

Marekani kuongeza ushuru bidhaa za China iwapo mazungumzo baina ya rais Xi Jinping na Trump hayatofikia muafaka

Rais Donald Trump wa Marekani amesema anafikiri kutakuwa na makuabaliano mazuri na China kuhusu biashara, lakini ameonya kwamba anaweza kuweka tena ushuru mpya wa mabilioni ya dola iwapo makubaliano hayatapatikana.

Kwa mujibu wa shirika la habari la DW, Trump ameyasema hayo kupitia mahojiano yake na kituo cha televisheni cha FOX News kwamba atapenda kupata makubaliano, lakini China bado haiko tayari.

Kituo cha televisheni cha Bloomberg kimeripoti jana kuwa Washington inajitayarisha kutangaza ushuru katika bidhaa zote za China zinazoingia nchini Marekani ifikapo mapema mwezi wa Desemba iwapo mazungumzo mwezi ujao kati ya Trump na mwenzake wa China Xi Jinping yatashindwa kupunguza vita vya kibiashara.

Marekani tayari imeweka ushuru katika bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 250, wakati China nayo imeweka ushuru wa dola bilioni 110 kwa bidhaa za Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents