Habari

MAREKANI: Shirika la upelelezi la FBI laeleza lilivyomtambua muuaji katili zaidi duniani – Video

MAREKANI: Shirika la upelelezi la FBI laeleza lilivyomtambua muuaji katili zaidi duniani - Video

Shirika la upelelezi la Marekani FBI limethibitisha kuwa mfungwa muuaji amekiri kuwaua watu 93 miongo minne iliopita ni mhalifu hatari zaidi katika historia ya nchi hiyo. Polisi imemhusisha Samuel Little na mauaji ya watu 79 katika visa 50 vya uhalifu wa aina hiyo kutoka mwaka 1970 hadi 2005 kufikia sasa.

Amekua akihudumia kifungo cha maisha gerezani tangu mwaka 2012 baada ya kupatikana na kosa la mauaji ya wanawake watatu.

Little aliwalenga hususan wanawake weusi ambao baadhi yao walikua makahaba na watumiaji wa dawa za kulevya, maafisa wanasema.

Bondia huyo wa zamani alikuwa akiwapiga ngumi waathiriwa wake kabla ya kuwanyonga – kumaanisha mara nyingi hakuna ushahidi wa “kudhibitisha” kuwa mtu aliuawa kikatili.

Baadhi ya vifo hivyo havikuchunguzwa na FBI na vingine vilidhaniwa kutokana na ajali au sababu zingine. Miili mingine haikuwahi ikipatikana, shirika hilo linasema.

Katika taarifa yake ya siku ya Jumatatu, FBI ilisema wachunguzi wake wanaamini ushahidi wake “wote ni wa kweli”.

“Kwa miaka mingi, Samuel Little aliamini hatawahi kujulikana kwa sababu hakuna mtu aliwatafuta waathiriwa,”mchambuzi wa masuala ya uhalifu wa FBI, Christie Palazzolo alisema katika taarifa hiyo. “Japo tayari ni mfungwa, FBI inaamini ni muhimu kuwatafutia haki waathiriwa – wa karibu kila kesi.”

Maafisa wa usalama bado wanachunguza visa 43 vya mauaji aliyokiri kutekeleza.

Samuel Little
Sumel Little, pia alijitambulisha kwa jina la Samuel McDowell
Maafisa sasa wametoa habari zaidi kwa umma kuhusu visa vitano vya mauaji yaliotekelezwa katika miji ya Kentucky, Florida, Louisiana, Nevada na Arkansas ili kusaidia utambuzi wa waathiriwa ambao hawajathibitishwa.

Shirika hilo awali lilisambaza michoro ya waathiriwa wa mauaji ya Little, ambayo alichora akiwa gerezani katika juhudi za kuwatambua waathiriwa zaidi.

Pia walichapisha kanda fupi za video wakati wakimhoji hasa sehemu aliyoelezea kwa kina jinsi alivyotekeleza mauaji hayo.

Katika moja ya visa vitano vinavyochunguzwa FBI inaomba ushirikiano wa umma kumtambua, mwanamke mwenye asili ya kiafrika kwa jina Marianne au Mary Ann aliyeishi Miami na Florida, mwanzoni mwa miaka ya 70.

Little alielezea jinsi alivyomuua mwanamke huyo wa miaka 19-karibu na shamba la miwa na kisha kuuburuta mwili wake na kuutupa katika shamba hilo.

Katika kisa kingine, Little alisimulia jinsi alivyomkaba koo na kumuua mwanamke mwingine mwaka 1993 katika chumba cha hoteli mjini Las Vegas.

Anakumbuka kukutana na mwanawe wa kiume na hata kusalimiana nae. Baada ya kumuua mwanamke huyo aliusafirisha mwili wake hadi viungani mwa mji na kuutupa katika eneo la mteremko.

Map of deaths linked to Little from FBI data

Maafisa wanasema kumbu kumbu ya Little ya mauaji hayo ni kidogo lakini anakumbuka tarehe halisi aliyovuruga uchunguzi.

Haijabainika ikiwa Little atafunguliwa mashitaka mapya kutokana na kukiri kutekeleza mauaji hayo..

Little alikamatwa mwaka 2012 na kushitakiwa na kosa la utumizi wa dawa za kulevya mjini Kentucky na kupelekwa hadi California, ambako maafisa walimfanyia uchunguzi wa chembe chembe za vinasaba, DNA.

Kwa mujibu wa BBC. Little alikuwa na rekodi mbaya ya uhalifu iliyojumuisha wizi wa mabavu na ubakaji katika maeneo tofauti nchini Marekani.

Matokeo ya uchunguzi wa DNA ulimhusisha na mauaji ya watu watatu ambayo uchunguzi ulifanywa mwaka 1987 hadi 1989 mjini Los Angeles japo haukua umekamilika. Alikanusha mashitaka hayo lakini alihukumiwa kifungo cha maisha gerzani.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents