Aisee DSTV!

Marekani: Tuhuma za agizo la kumpiga risasi 50 Cent zatupiliwa mbali

Uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba afisa mmoja mkuu wa polisi aliwaambia wenzake wampige risasi 50 Cent popote watakapomuona umefungwa.

50 Cent on stage

Marekani: Tuhuma za agizo la kumpiga risasi 50 Cent zatupiliwa mbali, uchunguzi wafungwa

Naibu inspekta Manuel Gonzalez alishutumiwa kwa kutoa matamshi katika hafla ambayo rapa huyo maarufu Marekani jina halisi, Curtis Jackson alitarajiwa kuhudhuria.

Tuhuma hizo zilitajwa “kutokuwa na msingi” na kesi imefungwa, Luteni Thomas Antonetti ameiambia BBC Radio 1 Newsbeat.

Instagram post by 50cent: I knew they were not going to do anything about this,so I stop talking about it. NYPD is hands down the toughest gang in New York. You just gotta be ready for what ever. You know the vibes. #TheKing🍾 #lecheminduroi #bransoncognac

50 Cent alisema: “Nilijua kuwa hawatofanya lolote kulihusu hili. Nikaacha kulizungumzia. NYPD kwa wepesi ndio genge kali New York,” aliongeza kwenye mtandao wa Instagram.

Ilidaiwa kuwa naibu Inspekta Gonzalez alitoa matamshi hayo na kujaribu kuyafanya kama mzaha, lakini aliripotiwa kwa idara ya mambo ya ndani ya NYPD.

Image result for 50 Cent vs Manuel Gonzalez

Mwezi mmoja kabla ya tukio hilo kutuhumiwa kufanyika, afisa huyo wa polisi aliwasilisha malalamiko dhidi ya 50 cent ya kudai kunyanyaswa vikali.

Alisema rapa huyo alimtishia kwenye mtandao wa Instagram katika kujibu tuhuma kuwa naibu inspekta Gonzalez alichunguza kwa upendeleo mojawapo ya vilabu vya burudani anavyopendelea kwenda 50 Cent.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW